Italia Yapiga Hatua Moja Karibu na Kombe la Dunia 2026 Baada ya Kuichapa Ireland ya Kaskazini

Timu ya taifa ya Italy imepata ushindi muhimu wa mabao 2-0 dhidi ya Northern Ireland katika hatua ya nusu fainali ya mchujo wa kufuzu kombe la Dunia 2026. Ushindi huo umeiweka Italia hatua moja tu kufuzu michuano hiyo mikubwa inayotarajiwa kufanyika Marekani, Canada na Mexico.

Italia Yapiga Hatua Moja Karibu na Kombe la Dunia 2026 Baada ya Kuichapa Ireland ya KaskaziniMchezo huo uliochezwa katika jiji la Bergamo ulikuwa mgumu katika kipindi cha kwanza huku timu zote zikishambuliana bila kupata bao. Hata hivyo, Italia ilirejea kipindi cha pili ikiwa na kasi mpya na kuanza kuonyesha ubora wake.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Kiungo Sandro Tonali aliifungia Italia bao la kwanza dakika ya 56 kabla ya mshambuliaji Moise Kean kuongeza la pili dakika ya 80 na kuhitimisha ushindi huo muhimu kwa Gli Azzurri.

Italia Yapiga Hatua Moja Karibu na Kombe la Dunia 2026 Baada ya Kuichapa Ireland ya KaskaziniKwa ushindi huo, Italia sasa itakutana na Bosnia na Herzegovina katika fainali ya mchujo itakayochezwa Jumanne ijayo. Bosnia ilitinga hatua hiyo baada ya kuiondoa Wales national football team kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.

Katika matokeo mengine ya hatua hiyo ya mchujo, Sweden iliichapa Ukraine 3-1 huku Poland ikiifunga Albania 2-1. Nayo timu ya Taifa ya Uturuki ilishinda Romania 1-0, wakati Kosovo ikiibuka na ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Slovakia.

Italia Yapiga Hatua Moja Karibu na Kombe la Dunia 2026 Baada ya Kuichapa Ireland ya KaskaziniTimu nyingine zilizopata ushindi ni Denmark iliyoifunga North Macedonia 4-0 pamoja na Czech Republic iliyoshinda kwa penalti 4-3 dhidi ya Ireland baada ya sare ya 2-2. Washindi wa mechi za fainali zijazo watajihakikishia tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia 2026.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.