Shirikisho la Soka Duniani FIFA limeutangaza rasmi Uwanja wa MetLife uliopo New York/New Jersey kuwa mwenyeji wa mechi ya fainali ya Kombe la Dunia 2026, itakayochezwa Julai 19, 2026.
Uwanja huo wenye uwezo wa kubeba zaidi ya mashabiki 82,000 umechaguliwa kutokana na ubora wa miundombinu yake ya kisasa pamoja na ukaribu wake na Jiji la New York, moja ya miji mikubwa na yenye ushawishi duniani.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kwa mujibu wa FIFA, uchaguzi wa MetLife unaendana na lengo la kuhakikisha fainali ya mashindano hayo makubwa zaidi ya soka duniani inafanyika katika mazingira bora na yanayokidhi viwango vya kimataifa.
MetLife si mgeni katika kuandaa matukio makubwa ya kimataifa, kwani tayari umewahi kuwa mwenyeji wa mechi ya fainali ya Kombe la Dunia la Klabu 2025.
Katika fainali hiyo iliyochezwa Julai 13, 2025, klabu ya Chelsea iliibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya PSG, katika mchezo uliovuta hisia za mashabiki wengi duniani.
Uamuzi wa kuuchagua uwanja huo unaongeza matarajio makubwa kwa mashabiki wa soka duniani, huku ukitarajiwa kushuhudia fainali yenye ushindani mkubwa na maandalizi ya kiwango cha juu yatakayoweka historia mpya katika Kombe la Dunia 2026.

