Infantino Athibitisha Iran Kushiriki Kombe la Dunia Licha ya Mvutano wa Kivita

Rais wa FIFA, Gianni Infantino, amesisitiza kuwa timu ya taifa ya Iran itashiriki Kombe la Dunia kama ilivyopangwa licha ya mvutano wa kivita unaoendelea katika ukanda wa Mashariki ya Kati.

Infantino Athibitisha Iran Kushiriki Kombe la Dunia Licha ya Mvutano wa KivitaInfantino alitoa kauli hiyo wakati wa mechi ya kirafiki iliyopigwa nchini Turkey, ambapo Iran iliibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Costa Rica.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

“Iran watakuwepo Kombe la Dunia. Ndiyo maana tuko hapa. Ni timu imara sana na nina furaha kubwa,” amesema Infantino, akionyesha kujiamini juu ya ushiriki wa taifa hilo kwenye michuano hiyo mikubwa.

Infantino Athibitisha Iran Kushiriki Kombe la Dunia Licha ya Mvutano wa KivitaAidha, Infantino  alibainisha kuwa ratiba ya mechi za Iran haitabadilika na itaendelea kama ilivyopangwa, huku michuano hiyo ikitarajiwa kuanza Juni 11 katika mataifa ya United States, Mexico na Canada.

Kwa mujibu wa upangaji wa makundi, Iran ipo Kundi G na itaanza kampeni yake dhidi ya New Zealand Juni 15 jijini Los Angeles, kabla ya kukutana na Belgium Juni 21 na kumalizia hatua ya makundi dhidi ya Egypt Juni 26.

Infantino Athibitisha Iran Kushiriki Kombe la Dunia Licha ya Mvutano wa KivitaMakamu wa Rais wa Shirikisho la Soka la Iran (FFIRI), Mehdi Mohammad Nabi, amesema “Kinachotuhusu zaidi ni kanuni za FIFA. Tutafuata kila watakachoamua. Nchi mwenyeji pia zina wajibu wa kutimiza makubaliano yao,” huku Claudia Sheinbaum akisisitiza kuwa Mexico iko tayari kuandaa mechi za Iran endapo hali ya usalama itahitaji mabadiliko.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.