Jurgen Klopp anapania kuwapa Liverpool Taji la kwanza baada ya miaka 29. Klopp anaamini yeye na kikosi chake huu ndio wakati wao wa kumaliza kiu ya taji klabuni hapo baada ya kipindi hiki kirefu. Klopp amesisitiza msingi mzuri wa kikosi chake ili wapate taji hili.
Liverpool wamefanikiwa kuna nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 2 tu zaidi dhidi ya Manchester City ambao bado wana gemu moja mkononi.
Ili Liverpool waendelee kukaa kileleni, lazima wamuombee njaa Mancity apoteze gemu yake aliyonayo mkononi kisha washinde gemu zingine zote zilizobakia kujihakikishia nafasi ya kusalia kileleni, sare au kichapo kwenye gemu yeyote inaweza kuwashuhudia wakipigwa gemu na Man City kama nao watakuwa imara kwenye gemu zao zinazofuata.
Man City watasafiri kuelekea Fulham Jumamosi wakiendeleza jalamba kwenye Ligi kuu ya Uingereza baada ya likizo ya kimataifa, wakati Liverpool watakuwa wenyeji wa Tottenham siku inayofuata, Man City ndiye anaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kupata ushindi.
Klopp anasisitiza kuwe na msingi mzuri kwenye wiki za mwisho ili wasiweze kutetereka kwa lolote. Anaamini hakutakuwa na kitu cha kuwakwamisha tena itakuwa ni kazi kazi huku wakiwa na vibarua vingine kwenye ligi ya Mabingwa Ulaya.


isha
Safi sana klopp