Klabu ya Manchester United inadaiwa kubadilisha mipango yao ya uhamisho, wakipanga kuwatazamia zaidi vijana kwenye sera yao ya uhamisho kwenye madirisha yajayo ya uhamisho.
Kwa mujibu wa chanzo cha taarifa cha ESPN FC klabu hii imeamua kubadilisha baadhi ya uelekeo wa usajili na kuwaangazia zaidi vijana wa miaka ya katikati ya 20 hivi, isipokuwa kwa Alexis Sanches na Nemanja Matic ambao ndiyo wachezaji wakongwe wanaofukuziwa.
Ole Gunnar yupo kwenye nafasi kubwa ya kuuchukua umeneja wa kudumu klabuni hapo, United wanatarajia kushirikiana na meneja wa kudumu klabuni hapo katika kutengeneza kikosi bora zaidi kupitia madirisha ya usajili yanayofuata.
Ripoti zinasema matarajio ya Ole Gunnar akiwa meneja klabuni hapo, ambayo pia ndiyo matarajio ya klabu ya Manchester United ni kutengeneza kikosi cha vijana ambao wananjaa ya kufanya mambo makubwa klabuni hapo, chipukizi ambao watakuwa na hamu zaidi ya kuionesha dunia kuwa wao ni bora zaidi katika ulimwengu wa soka kuliko kuwachukua wale ambao wameshatumika sehemu zingine kwa mda mrefu.
Mpango kama huu unatajwa kuwa mpango ambao uliwahi kuwekwa mezani na meneja wa zamani Sir Alex Ferguson miaka ya 2000 wakiwa wanalipa ada ya kawida kuwachukua wachezaji wa umri wa miaka 27 kushuka. Baada ya kuondoka meneja huyu United walianza kununua wachezaji ambao wenye umri ulioenda kidogo akiwemo Sanchez akiwa na miaka 29 wakati huo, Matic (29), Schweinsteiger (30) na Zlatan Ibrahimovic (34).
Hata hivyo, Ole Gunnar bado hajathibitishwa kuwa meneja wa kudumu, huenda taarifa njema za kumtunza meneja huyu klabuni hapo zikasikika mapema siku za usoni.


Furahav
Hii iko vizuri.