Rasmi Solskjaer Alamba Dili Kudumu United!

Kama ilivyokuwa matarajio ya wengi, na ilivyokuwa hamu ya wapenzi wa Manchester United ambao wanamsapoti aliyekuwa meneja wa mda mfupi Ole Gunnar Solskjaer, hatimae meneja huyu amechaguliwa kuwa meneja kwa miaka 3 zaidi kwa vigogo hawa wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Manchester United wametangaza kumpatia mkataba wa miaka mitatu Ole Gunnar kufuatia historia yake na klabu pia mafanikio aliyoyapata klabuni hapo kwa kipindi kifupi alichoitumikia klabu hiyo.

United wakiwa chini ya Ole Gunnar walianza kwa kushinda gemu 14 kati ya gemu 19 na kupoteza gemu moja tu kwenye Ligi Kuu ya Uingereza. Pia katika kipindi hiki United wamepata matokeo mazuri wakishinda gemu dhidi ya Arsenal na Chelsea kwenye FA Cup. United walivunja historia pia kwa kuwapindua PSG kwa kuwachaba bao 3-0 kwenye mtoano wa timu 16 UCL, baada ya kufungwa mzunguko wa kwanza bao 2-0 wakiwa kwao.

United wamevunja ukimya baada ya mda wa kimya wa kutomtaja meneja rasmi wa kudumu wa klabu hiyo. Ole Gunnar Solskjaer akishirikiana na Ed Woodward wanapanga kutengeneza kikosi cha wachezaji vijana ili kuwapa nafasi ya kukua ndani ya klabu na kuwa na uelewa na tamaduni za klabu.

Makala iliyopita

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.