Staa wa Manchester City, Raheem Sterling ameamua kuwafurahisha watoto wa shule aliyosoma zamani, kitaa tunaita Oldi Skuli. Nyota huyu ameamua kuwawezesha watoto katika shule hiyo ambayo aliisoma zamani kuhudhuria gemu ya Manchester City.
Raheem Sterling amenunua tiketi zipatazo 550 kwa ajili ya watoto hao kuingia dimbani Wembley kushuhudia mtanange wa mabingwa wa EPL Manchester City dhidi ya Brighton.
Neema hii itawafanya watoto wa Ark Elvin Academy watahudhuria gemu ya nusu fainali ya Kombe la FA. Staa huyu atawaandalia pia usafiri vyote vikiwa vimeandaliwa kwa kutoa fungu lake mfukoni.
Staa huyu mwenye miaka 24 amesema kuwa maisha yake kwa kiasi kikubwa yalikuwa ni hapo Wembley toka alipokuwa mtoto, maisha yake na mama yake yalikuwa mahali hapo na alikuwa anafurahia maisha yake akiwa shule hiyo aliyosoma. Ameona sio vibaya akiwafanyia kitu kizuri kuwafurahisha watoto hawa.


aisha
Raheem sterling amefanya vizuri
Mariam mtandama
Yupo vizur
Povel
Habar njema