Tottenham Hotspurs walikuwa wakisubiri kwa hamu sana kurejea kwenye uwanja wao mpya wa byumbani baada ya kucheleweshwa kwa mda kidogo. Bila shaka ilikuwa ni hamu kubwa ya klabu hii, hata ingekuwa nyingine yeyote kuzindua dimba lao la nyumbani kwa ushindi wa gemu ya kwanza kabisa uwanjani hapo. Machozi yalimwagika wakati wa kuuzindua uwanja huu wa Spurs!

Zaidi ya watazamaji 59000 walihudhuria gemu ya uzinduzi dhidi ya Crystal Palace jana kwenye uwanja huu wa unaokadiriwa kuwa na gharama ya paundi bilioni 1 wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 62000.

Shughuli nzima ilipambwa na miale ya baruti iliyopamba anga la dimba jipya la Spurs! Wapo mashabiki walioshindwa kuzuia hisia zao za furaha na kujikuta wakitoa machozi, ushindi wa gemu yao ya kwanza ulinogesha uzinduzi huu huku meneja Pochettino akijaribu kushindana na machozi yake kwa hisia za mchanganyiko wa furaha kwa namna alivyojisikia kuwa nyumbani na kupata ushindi wake wa kwanza hapo.

Son Heung-min na Christian Eriksen watakumbukwa kwa magoli yao yaliyowapaisha Tottenham kuendelea kuwa mbele ya Arsenal walio nyuma yao kwenye msimamo wa ligi.

Machozi Yalimwagika Dimba Jipya la Spurs

Ulikuwa ni usiku poa sana kwa mashabiki wa Spurs, huku Pochettino akiutaja ushindi huo kuwa ni heshima ya mwenyekiti Daniel Levy.

Pochettino
Heshima kwa Levy

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa