Maurinho ametajwa kuwa meneja anayefaa klabuni Inter Milan akitarajiwa ataweza kurejesha hali ya hewa kuwa shwari baada ya mvurugano wa hapa na pale klabuni hapo kufuatia sakata la Mauro Icardi.
Icardi alicheza gemu yake ya kwanza baada ya kama miezi miwili kupita, aliiongoza Inter kupata ushindi wa bao 4-0 dhidi ya Genoa huku wakifanikiwa kupanda hadi nafasi ya 3 kwenye msimamo wa Ligi Serie A.
Staa huyu aliwekwa kando kidogo toka alipovuliwa unahodha wa kikosi hicho sakata hilo likimhusisha zaidi mkewe ambaye pia ni wakala wa mchezaji huyu.
Bosin wa zamani wa Inter anafikiri huenda Mourinho akawa ndiye meneja atakayeweza kurejesha hali shwari pale Inter Milan kufuatia uzoefu wake na klabu hiyo. Meneja huyu anatambua kuwa kumrejesha Mourinho siyo kazi rahisi lakini anaamini inawezekana.


Povel
Habar njema