Huku EPL mambo yanaendelea kuwa matamu, Ligi inakuwa ngumu hapa mwishoni huku watabe Liverpool na Manchester City wakipambana kuchukua taji! Arsenal ameshindwa kuchomoka kwa Everton dakika 90 zimewaacha kapa huku Everton akisepa na ushindi mwembamba wa 1-0. Tunaweza kusema Sarri atakuwa amepata nafuu kidogo?
Wakati Man City na Liverpool wakiendelea kuviziana, Liverpool akimzidi pointi 2 tu Man City, vijana wa Guardiola wana matumaini ya kutumia mchezo walionao mkononi kuondoa gepu lililopo na kukaa kileleni kwa gemu 33 watakazokuwa wamecheza. akati huo Spurs ametulia katika nafasi ya 3 akiwa hana matumaini na taji.
Chelsea, Arsenal na Manchester United wanaendelea kufukuzana kwenye kiti cha nafasi ya 4 ili waweze kufuzu ligi ya Mabingwa. Arsenal alikuwa na nafuu ya gemu moja wakati kabla ya gemu hii wakiwa wanalingana pointi na Chelsea huku na akiikalia nafasi ya 4 kwa tofauti ya magoli.
Baada ya gemu hii
Arsenal walikuwa na nafasi ya kupigilia msumari nafasi yao kwenye ligi ya mabingwa kama wangeshinda gemu ya leo, wangemuondoa Spurs nafasi ya 3 na kuwatupa United na Chelsea.
Baada ya gemu hii nafasi ya 3 na 4 kwenye mpaka mwisho wa ligi bado zipo kwenye kinyang’anyiro kwa gemu kadhaa zilizokbakia. Solskjaer ana matumaini makubwa akihitaji kumaliza kwenye 4 bora katika msimu wake wa kwanza kama meneja.
Inaweza kuwa ni nafuu kwa Chelsea kama wakifanikiwa kushinda gemu inayofuata na kuwaombea njaa Arsenal katika gemu yao inayofuata, United yeye atakuwa nyuma ila wakivuruga wawili hao gemu zinazofuata yeye akatoboa basi atakuwa na kazi ya kuilinda nafasi ya 4 asipokonywe.



Furahav
Mmh
Povel
Mmh spurs vs United majanga kwl