Klabu ya Manchester United inaripotiwa kuwa wapo tayari kumnasa nyota wa Spurs Christian Ericksen ambaye atakula dili nono ikiwa atamwaga wino klabuni hapo.
United wanatajwa kuwa wapo tayari kumlipa staa huyu mara tatu ya mshahara wake anaolipwa sasa klabuni Tottenham Hotspurs.

Nyota huyu analipwa mshahara wa paundi 80,000 kwa wiki, United watamlipa mara 3 yake. Ni zali eenh? au mauwezo yake yana ruhusu!
Bosi Ole Gunnar Solskajaer amekuwa akisema kuwa kwa wapo kwenye makubaliano na makamu mwenyekiti Ed Woodward kuhusu mpango wa usajili pindi dirisha litakapokuwa wazi kiangazi, Ericksen anatajwa kuwa kwenye fikra za Ole Gunnar.
Bila shaka kumshawishi mwenyekiti Daniel Levy kumuuza nyota muhimu klabuni hapo haitakuwa kazi rahisi, United wanatambua hilo. Lakini mshahara anaolipwa sasa unafikiriwa kuwekwa mara 3 zaidi kumshawishi nyota huyu ambaye yupo kwenye mwaka wake wa mwisho klabuni hapo kabla mkataba wake haujaisha.


Povel
Gud news