Messi wa Japan Aliyetimba Madrid

Real Madrid wametangaza kumsainisha Takefusa Kubo ambaye alikuwa katika Akademi ya Barcelona na amekuwa akiitwa Messi wa Japan.

Staa huyu anayesa kutoka Tokyo ametajwa kuwa na thamani ya paundi milioni 2 na aliweza kucheza gemu kubwa akiwa na umri wa miaka 15 tu.
Kinda huyu ambaye sasa ana umri wa miaka 18 anatajwa kuwa mmoja wa vijana machachari sana wa kutoka bara Asia akionesha uwezo wake katika timu yake ya taifa ya Italia kwenye Copa America.
Kubo amekuwa mchezaji wa karibuni zaidi kusainiwa na Real Madrid na atawachezea timu ya pili Castilla kwa msimu ujao.

Zidane ana matumaini kuwa nba kikosi matata sana msimu ujao baada ya kuhakikisha wamenasa sahihi za wakali Eden Hazard, Ferland Mendy, Luka Jovic, Elder Militao na Rodrygo Goes.

Kinda huyu pia alikuwa anahusishwa na kurejea kwenye klabu iliyomlea akiwa akademi, Barcelona huku mabingwa wa Ufaransa PSG wakitajwa kumfukuzia pia. Klabu ya Real wamemtaja kuwa wamefanikiwa kumsajili mchezaji huyu kutoka Japan ambaye anakuja vyema sana kwenye tasnia ya soka.

2 Komentara

    Atafanya vizuri hapo madrid

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.