WrestleMania 35 kwa sasa ipo kwenye hatua zake za mwanzo kabisa ikiwa wengi wanasubiri kushuhudia mashindano yenye heshima kubwa na ushindani mkubwa sana. Ndani ya mashindano hayo wakongwe wengi wanajiandaa kuzishikilia rekodi zao na wengine wakitaka kuvunja rekodi zote zilizowekwa kwenye michuano ya nyuma.
Huku mbio hizo zikiwa zinaanza kupamba moto wa aina yake leo tutakurudisha nyuma kidogo kushuhudia baadhi ya mapigano bora kuwahi kushika nafasi ulingoni miaka ya nyuma pale wakongwe walipopata nafasi ya kupambana. Na ndani ya historia hizo walijenga ushindani wa kipekee hata mbele ya mashabiki wanaowazunguka.
Bret Hart [C] dhidi ya Shawn Michaels, waliweza kukutana kwenye pambano la kihistoria lilokuwa katika ngazi ya The WWF Championship. Mechi hiyo ilikuwa ni katika WrestleMania 12, kutokana na ugumu wa mechi ilihitaji muda wa ziada ili kuweza kuamua mshindi na jambo hilo lilimpa nafasi Michaels aliyeonekaba na ufundi zaidi ya wapinzani wake.
Bret Hart mbele ya Steve Austin, mwaka mmoja baada ya kupoteza mechi yake kutoka kwa HBK kwenye pambano lake la wrestlemania 12 aliweza kukutana na ingizo jipya kwenye mashindano hayo. Kwenye pambano hilo Austin aligeuka kipenzi cha wengi kutokana na makubwa aliyoyafanya na alivyowavutia wengi.
The Dudley Boyz [C] dhidi ya The Hardy Boyz na Edge na Christian, hii ilikuwa katika pambano lililopigwa likiwa ni la 17 kimashindano. Ndani yake lilitawaliwa na ubabe wa kila aina huku kila mmoja akitafuta namna ya kuondoka na ubingwa hapo. Ndani ya pambano hilo kulishuhudiwa Edge na timu ya akina Christian wakiibuka na ushindi wa taji hilo.
The Rock dhidi ya Steve Austin, walikutana kwenye mechi hiyo kubwa mbele ya shindano la WWF Championship kwenye wrestlemania 17. Wawili hawa walikuwa wanarudiana kwenye pambano hilo ikiwa ni kumbukumbu ya mechi yao iliyowahi kupigwa kwenye mlolongo wa mashindano hayo awali katika shindano la 15. Ndani ya mechi yao ilishuhudiwa The Rock akipokea kichapo kwa kiti mbele ya mpinzani wake huyo.
Shawn Michaels dhidi ya The Undertaker, hii ilikuwa katika WrestleMania 25 ambapo wawili hao waliweza kukutana ulingoni. Mbali na hatua hiyo iliweza kushuhudia Undertaker akipanda kwenye kamba za ulingo wa uwanja huo na kumvaa mpiga picha za tukio hilo jambo ambalo lilijaa vitimbwi vya kila aina. Na kilichoshuhudiwa baadaye ni Michael kukubali kipigo hicho na kumruhusu Taker kuondoka na ubingwa.
Hayo ni baadhi ya mapambano yaliyoweza kuwafurahisha na kujenga historia ulingoni kutokana na uwezo uliooneshwa na wanamieleka hao. Yapo mengi kutoka kwa watu kama John Cena, Baptista, Seth Rollins, Brock Lesnar hata Roman Reigns lakini hayo ni sehemu ya yale yaliyojenga historia.

