Timu ya taifa ya Ujerumani na klabu ya Bayern Munich ambayo inashiriki ligi nchini humo bado zina utegemezi wa hali ya juu kwa mlinda mlango Manuel Neuer ambaye ana rekodi ya aina yake ndani ya taifa na klabu hiyo. Lakini pamoja na uhitajikaji wake ndani ya timu hizo lazima itafika wakati atastaafu soka.
Nyota huyo anaona kwamba itafika wakati wa yeye kuachana na soka pale ambapo ataona kuhitajika kwake ndani ya timu ambazo yeye ni tegemeo kubwa umeweza kushuka. Hiyo inajumuisha klabu ya Bayern ambayo bado anashika nafasi ya kwanza kwa utegemezi ndani ya kikosi hicho.
Neuer mwenye umri wa miaka 33 bado anahitajika ndani ya kikosi cha Bayern amiwa kama chaguo la kwanza kabisa na hakuna mtu ambaye anaonekana kuchukua nafasi hiyo hivi karibuni. Umuhimu wake kikosini hapo ni tangu ajiunge na kikosi hicho mwaka 2011 ambapo amekuwa akifanya vyema sana na kikosi hicho kwa mafanikio makubwa sana.
Lakini nyota huyo aliyeibukia kutoka kituo cha mafunzo ya kisoka Schalke ameweza kukutana na changamoto za mara kwa mara kama mchezaji kutokana na majeraha ambayo yamekuwa yakimweka nje ya uwanja mara nyingi. Mfano msimu wa 2017/18 aliweza kukaa karibu msimu mzima nje kutokana na majeraha yake ya mguu aliovunjika.
Pamoja na hayo pia ameendelea kukumbana na majeraha ambayo yamemuweka nje ya uwanja kwa kipindi zaidi hasa yale ya vidole ambapo kwa walinda mlango huwa ni tatizo la kawaida sana kwao kukumbana nalo katika majukumu yao ya kila siku. Lakini majeraha hayo hayamnyimi nafasi ya kuwa chaguo la kwanza kikosini.
Kwa sasa anaamini kwamba itafika wakati atalazimika kustaafu soka kutokana na ushindani ambao utatokea. Anaona kwamba ikitokea pale ulipo ushindani upo chini kwako unalazimika kuweza kujishusha ili kuwapisha wengine ambao wanapanda kwenye nafasi hiyo kiushindani. Hilo ndilo litakalomweka nje katika kikosi hicho na katika nafasi hiyo.
Anaamini kwa wakati uliopo kila mtu anaufurahia uwepo wake kikosini hapo na kwake ni nafasi ya pekee kuweza kufanya yale ambayo hakuyatimiza alipokuwa kijana ndani ya timu hizo. Wakati huu anaamini ni wa yeye kutimiza njozi zake zote na kulipa fadhila ya yeye kuaminika na kupewa nafasi kikosini hapo.


Povel tz
Habar njema