Inadaiwa kuwa ligi kuu ya Ujerumani, Bundesliga inaweza kuwa ya kwanza kurejea uwanjani, hayo yamesemwa na waziri wa Ujerumani kwamba kuna mazungumzo yanayoendelea kwa sasa ili ligi irudi mapema mwezi Mei hasa tarehe 9 mwezi huo.
Ujerumani imeweza kupunguza madhara makubwa ya Coronavirus kwa sasa na wanaendelea kukazia udhibiti wa kwenye maduka kadhaa ya miji yao nchini kule, vibanda vya baiskeli na wauzaji wa magari wameshaanza kufanya kazi zao kama kawaida, lakini bado wanasisitiza juu ya kukaa umbali wa mita 2 kati ya mtu na mtu katika maeneo yao.
Kwa sasa inaonekana bayana kwamba ligi itarejea nchini humo ndani ya wiki kadhaa zijazo ingawa itakuwa ikichezwa bila ya uwepo wa mashabiki wao, katika hotuba yake waziri wa Ujerumani, Bwana Markus Soder alithibitisha kwamba wanazungumza na shirikisho la soka la Ujerumani juu ya kurudisha michezo ya soka iliyokuwepo mwanzo.
“Tunazungumza juu ya hilo na kila kitu kipo sawa kabisa,” alisema Soder.
“Wahusika wa DFL wametuthibitishia kwamba wanachukua tahadhari za ugonjwa huu wa mlipuko. Na ninaona wazi wazi kwamba tunaweza kucheza ingawa itakuwa ni bila ya uwepoo wa mashabiki wa soka.”
Amesema kwamba wanafanya juhudi zaidi ili kupambania suala hilo likae sawa. Kwa sasa wanatakiwa kuwa makini na kujitahidi kuzuia ugonjwa kadri iwezekanavyo. Gemu zikiwa na watazamaji zinawaweka hatarini na madhara yake ni makubwa sana. Lakini gemu kuchezwa bila ya mashabiki ni wazo jema sana kwa kweli.
Wikiendi bila gemu inaboa!
Anasema zaidi kuwa watatakiwa kucheza gemu bila ya mashabiki kuanzia mwanzo wa muendelezo wa michezo hiyo mpaka pale hali itakapokuwa sawa zaidi. Hiyo ni kuanzia Mei 9 mwaka huu. Anasema kwamba wikiendi kukiwa na michezo inaleta raha kuliko kuwa ila ya michezo yoyote ile.
Gemu za Ujerumani zilisimamishwa Machi 13 lakini baadaye klabu zikaruhusiwa kuendelea na mazoezi mapema mwezi huu, ingawa wanaenda kwenye mazoezi kwa makundi makundi ya watu watano watano na kuepuka kusogeleana sana uwanjani.
Endapo jambo hili likitimia basi ligi hii itategemewa kumalizika kabla au karibia na tarehe 13 mwezi wa Juni mwaka huu ambapo itakuwa ni kama pigo kwa klabu za Premier League kwa sababu wachezaji wengi mikataba yao inamalizika kipindi hicho.
Wanaokaa juu ya kilele ni Bayern Munich na watajaribu kutwaa taji lao kwa mara ya nane mfululizo dhidi ya mahasimu wao wa Borussia Dortmund ambao wanapishana kwa alama nne tu.
Lakini pia nao RB Leipzig wanawakaribia sana pia ambapo kuna upande wa Lucian Favre na wa Borussia Monchengladbach pia wakiwa katika msako mkali wa taji la ligi hiyo.
Na upande wa Premier League pia klabu nyingi zina salio la mechi nane ama tisa lakini wengine wana gemu 10 ili kumaliza msimu wao.
Chini kabisa tunawakuta akina Paderborn na Werder Bremen wanaosua sua na wanasaka sana kushinda kwani wana alama sita na nne kuelekea kushuka daraja.


Furahav
Itakuwa vizuri.