Ulishawahi kumsikia mtu mmoja anaitwa Alberto Fantarau? Jamaa ambaye Ronaldo anamtaja kuwa shujaa wa maisha yake. Alberto Fantarau alikuwa anakipiga na Ronaldo katika academy moja nyumbani kwao Ureno. Siku moja alikuja scout kutoka academy kubwa zaidi ya ile yao kumtazama Ronaldo na huyo rafiki yake Alberto. Ronaldo anasema huyo scout aliwakubali wote ila nafasi ilikuwepo ya mmoja wao. Hivo aliwaambia kwenye mechi siku hiyo yoyote atakayefunga magoli zaidi ya mwenzake atapata nafasi ya kujiunga na academy yao.

Ronaldo anasema walishinda tatu bila siku hiyo. Yeye (Ronaldo) alifunga bao la kwanza. Alafu Fantrau alifunga bao la pili kwa kichwa. Bao la tatu ndilo lilikuwa na mvuto zaidi. Fantrau alikuwa one on one na goalkeeper, kama ilivodhaniwa akampiga chenga, akabaki na nyavu, ila badala ya kufunga akageuka akanipa pasi nikauweka kwenye nyavu tupu. Hivo nikapata nafasi ya kwenda mbele.
Mechi ilipoisha nikamuuliza kwanini alifanya vile, akanijibu, wewe una uwezo kuliko mimi. utafika mbali zaidi yangu hivo nenda wewe. Waandishi wa habari walimtafuta Fantrau kuthibitisha ukweli wa maneno ya Ronaldo. Walimkuta ana maisha poa sana ya kifahari. Wakamuuliza ulipataje vitu vote hivi ilihali hukucheza mpira? Jibu lake lilikuwa rahisi. “Ronaldo”. Ronaldo alikuwa anarudi kwa jamaa yake kila mara kushirikiana nae mafanikio yake.
Ronaldo ametimiza miaka 35 leo. Fantrau atakuwa upande mwingine wa dunia anapata glass champagne akifurahia mafanikio ya rafiki yake. Atageuka nyuma na kutazama ile pasi ilipowafikisha. Hatakaa aijutie..


Furahav
Huo ndiyo urafiki bora duniani,na Alberto na Ronaldo wanafaa kuingwa na jamii.