Kabla Hujamfokea Messi, Geuka Mtazame Flick

Swali la kwanza kwa Barcelona ni kuwa, tatizo ni nini haswa? Jibu la swali la kwanza linaweza kuwa kipengele cha kwanza cha swali la pili. Tatizo lilianzia wapi? Kabla ya kulaumu matokeo, kabla ya kuulaumu mchezo, lazima ipo sababu iliyowafikisha Barcelona huku. Imekuwaje wakawa na timu mbovu namna hii?


.
Baada ya hapo unaweza kugeuka na kuuzungumzia mchezo. 8-2. Historia inaniambia hiki ndio kipigo kikubwa zaidi kwa Barcelona kwa miaka zaidi ya miaka 50 iliyopita. Nini kimesababisha? Ni wazi kocha Quique Setien aliangushwa na daftari lake la mbinu. Hata kama Barca hawana timu imara kwa sasa, bado hawakustahili adha kubwa namna hii.
.
Setien alijua Bayern Munich wana timu nzuri kiuchezaji kuliko yeye. Alijua wazi Bayern Munich wana wachezaji wazuri kuliko yeye. Ila bado hakuwaheshimu, alifunguka akataka kushindana nao kucheza mpira. Hata waliporudi kipindi cha pili, bado alithubutu kumtoa beki na kumuingiza mshambuliaji. Alimaanisha nini kufanya vile wakiwa bado wanaandamwa na mashambulizi? Setien alijichimbia kaburi lake mwenyewe. Ni suala la muda tu kabla hajapewa mkono wa kwa heri.

Wakati Setien anapewa mkono wa kwa heri nyuma yake Hans Flick atakuwa anapokea mkono wa pongezi. Amewezaje kuitengeza timu imara namna ile kutoka kwa wachezaji wa kawaida tu? Amewezaje kuwafanya wachezaji wa kawaida kuwa hodari namna ile? Huyu Sergie Gnabry alifeli England. Huyu Coutinho amefeli Barcelona. Huyu Goretzka alikuwa mtu wa kawaida tu pale Schalke 04. Amewezaje kuwabadilisha?

Ila bado namuhoji, Anakosa nini kwa yule Thiago Alcantara? Kwanini anataka kumuacha aondoke? Ajifikirie mara mbili. Si anajua akili nyingi huondoa maarifa? Vipi kuhusu yule mtoto? Yule Alphonso Davies. Kuna binadamu mwenye wasiwasi nae? Akikimbia nyuma ya mpira, akili yake anaiweka mbele ya mpira, halafu moyo wake anaufunga ndani ya mpira. Hafanyi kosa lolote, anakupa zaidi ya unachotaka. Yule mtoto🙌.


Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Basi fahamu kuwa kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.

Soma zaidi

39 Komentara

    Asante meridianbet kwa makala nzuri

    Jibu

    Barcelona kweli walijua kupokea kichapo jamn cjui tatizo lilikua nn mpk kukubali kipigo kikubwa zaidi ya miaka 50iliyopita#Meridianbettz

    Jibu

    Huyu kocha wa Barcelona alivyo fanya kama kocha wa yanga kwenye alivyo fanya hadi kuja kupelekea kufungwa magoli 4 na wapinzani wao simba fc aliwaacha wachezaji kawapanga mastaa kana wakana Morrison nk..!kikubwa asiangalie ustaa apange kikosi chake kwani Barcelona akuna wachezaji pale kuna mastaa tu

    Jibu

    Bonge la makala
    @meridianbettz

    Jibu

    Barca wametia aibu sana naona wanataka kuwa kama Barca ya miaka 50 ya nyuma kocha atulize kichwa ajue tatizo lipo wapi

    Jibu

    Hapo Barcelona na mashabiki ambao hatujui Moira tutaaza kumlaumu nahoza wa timu utasema alikuwa pekeyake uwanjani .tatizo lipo kwa viongozi wanatakiwa kuangalia kuwa timu yao iko kwa kiwango gani ili iwapange au kuongeza palipo pungua .katika nafasi aliyo toka nerymaa hakuna aliye paziba sana naona zipo nafasi mbili zaidi lakini haziwezi Fanya kitu mpaka ipate ngufu kutoka nafasi ya utatu yenye nguvu lakini sasa hamna kwa nini wasifugwe magoli 8 na kama dk zingeongezwa zaidi wangegombana wao kwa wao uwanjani fanyeni marekebisho kwanza mambo mengine yaendelee

    Jibu

    Kiukweli kile kipogo walichopokea barcelona sio Cha kawaida Ila sio mbay wajipange mchezo mwingin

    Jibu

    Oky kwanza poleni sana barcelona kwa kipigo mlichopata lakini mimi naamini kuwa huwezi kufanikiwa kwenye maisha yako kama hujapatia mitihani amabayo ni kama hiyo na lakini maneno ya wanadam achaneni nayo kwasababu hakuna asiyekosea wala aliyekamilika hapa duniani isipokua mungu peke yake na pia wanadam wanapenda siku zote ufanye mazuri tuu hivyo basi ukikosea baya moja wanasahu mazuri yako yote uliyoyafanya inshu ya msingi mjue wapi milifanya makosa na kuanzia hapo hapo ili mambo yakae sawa achana na wanadam wasio kuwa na shukurani #meridianbet

    Jibu

    Asante kwa makala nzuri

    Jibu

    Kiukweli kile kipogo walichopokea barcelona sio Cha kawaida Ila sio mbay wajipange mchezo mwingin

    Jibu

    Hayo yote ni moja ya matokeo kwenye mchezo,jipangeni upya!!!

    Jibu

    Hakuna haja ya kulaumiana.waangalie wapi walipokosea wajipange upya

    Jibu

    Makala imetulia sana

    Jibu

    Barcelona waache maneno maneno wanatakiwa kukaa chini na kujitasmini kwa makini huu sio mda wa kulaumiana

    Jibu

    kwa kipigo kile sidhani kama barcelona watakuja kusahau 🤣🤣🤣

    Jibu

    Kwenye Soka kuna kitu kinaitwa kuamka vizuri au Bahati, Kwanza Bayern walikuwa kwenye form maradufu kuanzia kipa adi wachezaji wote ndani, Mbinu za Mwalimu na juhudi za mchezaji mmoja mmoja ndio chachu ya ushindi mkubwa dhidi ya Barca, Barca ilikuwa zaidi ya Utopolo Fc, Hashakumu si matusi lakini.

    Jibu

    Amna swala kumuangalia Nani kakosea au yule kapatia krabu Kama krabu inaweza ikaa Chini nakuzungumza apa tumekosea nijambo lakulekebishwa sio kumuambia mtu kakosea Messi kakosea Flick kakosea amna kitu hicho usimshutumu mtu kosa nilakulekebishwa kwawote nasio mmoja inatakiwa timu Kama timu kukalishwa Chini kuzungumza kwaujumla

    Jibu

    Barcelona ya sasa haikuwa na uwezo wa kuizuia Bayern inayocheza kitimu pamoja na ubovu huo haikutarajiwa ifungwe 8. Ni kipigo cha aibu.Kama alivyosema Gerrard Pique kwamba Barcelona inahitaji mabadiliko makubwa ya bench la ufundi na wachezaji#meridianbettz

    Jibu

    Barcelona wanayumba sana hiki sio kipindi cha kujilaumu wanatakiwa wajipange

    Jibu

    Mbinu nyingi ndio zinakupa matokeo Luna msemo wa bongo wansema ukisema cha nini wengine wanawaza ntakipata lini hii ndio imewatokea barca kumtoa countinho fundi was kibrazil mwenze uwezo mkubwa sanaa kumuona kuwa hafai ila siwezi mllaumu kocha nageuka kwa messi huyu ndio shida na kufanya timu kuwa mbovu

    Jibu

    Mpira siku zote hua inamatokeo ya ajabu Sana kwa upande wa Bayern walikua bora zaidi ya Barcelona na walistahili kupata walichokua wanakitaka.

    Jibu

    Hapo Barcelona wamehalibi sana na kwa upande wa mabeki hawana kabsaa

    Jibu

    Bayern walikua na siku nzuri Sana kwenye hii mechi na wakadhihilisha kwamba wao wana kikosi kipana na bora kuliko barca.

    Jibu

    Kuna kuzidiwa kimbinu hiko bayern ndio waliwazid barcelona hamna kingine zaid

    Jibu

    Wanakosea kumtetemesha mess

    Jibu

    Nimeikubali hii makala.

    Jibu

    Barcelona hata wangejipanga vp wasingeweza kuzuia kichapo kutoka kwa Bayern Ila kwa gori 8 kweli ni zaidi ya fedheha

    Jibu

    Duh!

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

    Wajerumani siyo watu wazur

    Jibu

    Kwenye Soka kuna kitu kinaitwa kuamka vizuri au Bahati, Kwanza Bayern walikuwa kwenye form maradufu kuanzia kipa adi wachezaji wote ndani, Mbinu za Mwalimu na juhudi za mchezaji mmoja mmoja ndio chachu ya ushindi mkubwa dhidi ya Barca, Barca ilikuwa zaidi ya Utopolo Fc, Hashakumu si matusi lakini.

    Jibu

    Kwa kweli Barca Kipindi hiki kiwango Kipo chini sana#Meridianbettz

    Jibu

    hakuna wa kumlaumu zaidi ya kocha akuwapanga vizuri wachezaji wake mpaka kufikia kupokea kichapo cha aibu kubwa

    Jibu

    Habari imeeleweka

    Jibu

    Hii mechi hata sio ya kuzungumzia ukiachana tu na matatizo ya barca waliokua nayo ila sio kufungwa goli nyingi kama hizi.

    Jibu

    Siku zote mpira hubadilika na muda mwingine ata kama timu nzur sana unaweza siku ikatokea mpira umekukataa siku hiyo mbona tunaona hata timu kubwa inafungwa na timu ndogo sio swala la kumlahumu kocha

    Jibu

    habari njema

    Jibu

    Duuuuh hatari

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.