Sancho Afurahia Maisha ya Dortmund

Winga wa Klabu ya Borussia Dortmund, Jadon Sancho amesema kuwa “anafurahi sana” kushirikiana na wachezaji wachanga wa Klabu hiyo na anataka kusaidia kuwaongoza – Winga huyo wa kimataifa England mwenye umri wa miaka 20, ndiye chaguo la kwanza msimu huu wa joto kusajiliwa na Manchester United.

Lakini Mkurugenzi wa Michezo wa Dortmund, Michael Zorc alisema Jumatatu Sancho ataendelea kusalia kwenye Klabu hiyo ya Ujerumani msimu ujao.

“Ninafuraha na maisha ya hapa,” alisema Sancho baada ya kuanza maandalizi kwa mchezo wa kirafiki Buki nchini Uswisi, wote pamoja na Jude Bellingham na Gio Reyna wenye umri wa miaka 17 wakicheza mechi hiyo.

“Sisi ni kundi maalumu. Tuna wachezaji wachanga maalumu wanaochipukia, Nimefurahia sana kushirikiana nao na kuwaongoza”.

“Nilijiunga nilipokuwa na umri wa miaka 17 – baadhi ya wachezaji wengine wana umri kama huo, Nimekuwa hapa na nimefanya vema. Naweza kuwaongoza katika kile kizuri na kisichosawa kufanya, Naweza kuwahimiza kwa matumaini pia.”

United ni kama wameshindwa Kumsajili kinda huyo wa zamani wa Manchester City, kwani wanadhani dau wanalotaka Dortmund takribani £100m, mshahara wa mchezaji na ada ya wakala yote ni ya juu sana kutokana na athari ya kifedha baada ya janga la COVID-19 – Tarehe 10 Agosti ilikuwa ndio mwisho wa klabu hiyo ya Bundesliga kupokea ofa kuhusu uhamisho wa Sancho.


Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Basi fahamu kuwa kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.

Soma zaidi

35 Komentara

    Safi

    Jibu

    Sancho yupo sawa me sioni haja ya kwenda clabu yengine ikiwa bado hanafasi nzuri tu pale Dortmund kama mchezaji tegemezi mwenye uwezo kwa kiasi..!

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Sancho Yuko vizuri na anawafurahia wachezaji wezanke na umoja Ni nguvu siku zote@meridianbettz

    Jibu

    Sancho ni mchezaji anae juwa na hakuna timu ambayo ingemkataa yeye ila kwa sababu yeye anapenda kuendelea Dortmund basi tunaheshimu maamuzi yake

    Jibu

    Sancho yupo sahihi anaamani na mahala alipo ni vizuri hata kazi zako unakuwa unafanya ki uhuru

    Jibu

    Sancho ni mchezaji mzuri halafu anachokiamini kuwa furaha ndio mafanikio yake hauwezi kuchezea club ambayo hauipendi inamaana utakosa mafanikio kwa kutokipenda kitu nakutakia mafanikio mema

    Jibu

    Sancho Ni mchezaji mzuri sana mm sioni haha ya kwenda kwenda club nyingine

    Jibu

    Sancho Ni mchezaji mzuri San na nibora abaki club yake

    Jibu

    Sancho tulia tuu upo sehemu salama!!!

    Jibu

    Safi sana.ni vizuri kua na furaha na unachofanya.inaongeza ufanisi wa kazi

    Jibu

    Dortmund pazuri, abaki hapo hapo.

    Jibu

    Sancho ni mcgezaji anajielewa na kupenda kushikiliana na wezake kwenye mazoez

    Jibu

    always umoja ni nguvu utengano ni dhaifu

    Jibu

    Safii Sana Sancho kwa maisha ya Dortmund Uzidi kupambana iliufikie malengo yako

    Jibu

    Man U wanatakiwa kutafuta Mbadala wa Sancho maana kila siku habari mpya

    Jibu

    Nadhani Sancho anatakiwa kufikiria mara mbili mbili kuondoka Dortmund iliyomupa nafasi ya kucheza na kujulikana. Coutinho mpaka leo atakuwa anajuta kuondoka Liverpool iliyomupa nafasi ya kucheza na kujulikana kila mahali. Dortmund ndio mahali sahihi kwake kuwepo#meridianbettz

    Jibu

    Safi sana kula maisha dortmund

    Jibu

    Pesa nyingi sana ambayo wanaitaka kwa Sancho man wanatakiwa kuachana klna Jordan Sancho na kuangalia wachezaji wenye uwenzo mkubwa na wapo kwenye vilabu vidogo vidogo

    Jibu

    Kwa maneno haya wale makocha waliokua wakiwania kandarasi yake waangalie sehemu nyengine.

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Kwa vilabu ambavyo vilikua na kiu na Sancho hasa man u wajipange upya kwa msimu ujao.

    Jibu

    Ni noma sana

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Sawa

    Jibu

    Ole lengo lake kubwa alikua ni kumpata Sancho kutokea dortmund

    Jibu

    Gud to hear this

    Jibu

    Gud

    Jibu

    Nadhani Sancho anatakiwa kufikiria mara mbili mbili kuondoka Dortmund iliyomupa nafasi ya kucheza na kujulikana. Coutinho mpaka leo atakuwa anajuta kuondoka Liverpool iliyomupa nafasi ya kucheza na kujulikana kila mahali. Dortmund ndio mahali sahihi kwake

    Jibu

    Mda mfupi tu kesha anza kufurahia!Duuu huyu atakuwa muongo!#Meridianbettz

    Jibu

    united wameshindwa kumnyakua sancho sidhani kama nafasi iyo itakuja kupatikana tena

    Jibu

    Hapa ole gunar ameshafel kabisa maana n mchezaji ambaye alikuwa na ndoto nae kikosin

    Jibu

    sancho namkubali sana

    Jibu

    Habari njema Sana

    Jibu

    Safiii

    Jibu

Acha ujumbe