Lionel Messi ameelezea umuhimu wa kupata ushindi na sio swala la kuonesha kiwango baada ya Argentina kucheza mchezo wao wa kufuzu kucheza World Cup kwa kuichapa Ecuador 1-0
Messi kwa mara nyingine alikuwa shujaa kwa timu ya Argentina katika dimba la Buenos Aires siku ya Alhamisi kwa kufunga penati waliyoipata dakika ya 13 kwa mara ya kwanza tangu walipofanya hivyo mwezi Novemba mwaka uliyopita.

Ratiba ya mchezo wa Argentina kuanza mbio za kufuzu kushiriki fainali za kombe la dunia mwaka 2022 nchini Qatar ilipangwa kutimua vumbi mwezi Machi, lakini kutokana na kuzuka kwa janga la Corona mipango yote ilikatishwa.
Miamba hiyo ya Amerika ya kusini hatimaye walirejea dimbani na kuendeleza rekodi yao ya kutofungwa katika michezo nane waliyocheza na pongezi nyingi zilimuendea nyota na mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or mara sita, Lionel Messi.
“Tulikuwa tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini kitu cha umuhimu ni kwamba tumeshindaa na sasa tunapaswa kuangalia mbele na kufanyia kazi palipo pwaya,” Messi alisema baada ya mechi kuisha.
“Ilikuwa ni muhimu kupata ushindi kwa kuanza sababu tunajua ugumu uliyopo kwa timu zote zinazo taka kufuzu kucheza kombe la dunia.
Messi na wenzake walicheza bila uwepo wa mashabiki katika dimba la La Bombonera kutokana na uwepo wa janga la COVID-19.
Kuna visa zaidi ya 856,000 vilivyoripotiwa mpaka sasa na vifo zaidi ya 22,700 katika taifa la Argentina.
“Ulikuwa ni mwaka mgumu ambao tumeupitia,” alisema Messi wa Barcelona ambaye pia timu yake ya taifa itakutana na Bolivia siku ya Jumanne.
Sasa unaweza kuweka pesa moja kwa moja kwenye akunti yako ya Meridianbet kwa kutumia mtandao wa Airtel. Usipate wasi wasi, tunaifanya kazi kuwa rahisi zaidi!


Shani
Mess umr umesonga
Ernest
Wachezaji wa Argentina wanatakiwa kujituma zaidi sio kumtegemea tuu Messi
Samira
Wachezaji wengine wanatakiwa kuonyesha ushirikiano sio macho yote wanamtolea macho Messi tu
magdalena
messi yupo sahihi sana na anachokisema ushindi ni muhimu sana kulinda heshima ya timu kikubwa kushirikiana
Caroline
Messi ana akili sanaa
Adelta
Messi anamaarifa mengi
Sauda
Messi yupo sahihi kabisa
Mwanahamisi
Messi ni jembe
Fatina mfigi
Messi Ni kichwa
Neema
Messi ni nomaa
Saupha mohamed
Messi yupi sahihi ushindi ndo heshima
Angelina
Messi mtu mbayaa
Samiah
Mtu makini sanaaa Messi
lombo
hana jipya
Fatuma kasomo
Mess yupo vizuri
Povel
Kwl CAPTAIN Messi🖐️🖐️
Hopemwaikuka
Messi namuelewa
David Pere
Wachezaji wa Argentina wanatakiwa kujituma zaidi sio kumtegemea tuu Mess
Lydia Emmanuel Magoti
Nikweli Messi anajitiada nyingi tuu zakuipa Argentina ushindi wakila namna
Rehema
Anatakiwa apambane tuu
Sabrina
Messi anajua mpira
aisha
Mess anahitaji nguvu zaid ili afanye maajabu kwenye mpira
Amiri Kayera
Ni kwer cha kwanza ushind mengne Extraa
latifa juma mohamed
Messi fundiii.
Gabriel
Messi ni jembe
Rose kapinga
Kweliii