Ntibazonkiza, Kaze Amefanya Nisaini Yanga

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Said Ntibazonkiza, amesema timu hiyo ilianza kumfuatilia miezi miwili hadi mitatu iliyopita kabla ya kufikia makubaliano ya kusaini mkataba huku akitamba ametua kwa kazi moja tu ya kusaidia timu kutwaa mataji.

Ntibazonkiza alisajiliwa na Yanga Oktoba 12 kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu akiwa mchezaji huru ambapo vijana hao wa Jangwani walimnasa baada ya kumalizika mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Tanzania dhidi ya Burundi uliomalizika kwa Burundi kupata ushindi wa bao 1-0.

Bao la ushindi kwa Burundi ambalo liliacha ganzi kwa Watanzania Uwanja wa Mkapa, Oktoba 11 lilifungwa na yeye mwenyewe Ntibazonkiza.

Kwa mujibu wa Ntibazonkiza amekiri ujio wake katika timu hiyo, kocha mpya Cedric Kaze amehusika kwa asilimia mia moja kutokana na kuwahi kumfundisha kwenye timu ya Taifa ya Burundi, mwaka 2011.

“Mimi nimekuja Yanga sio kwa bahati mbaya, wapo wanaofikiria nimesajiliwa baada ya mchezo dhidi ya Tanzania.

“Tulikuwa na mazungumzo na Yanga miezi miwili au mitatu nyuma.Lakini nilishindwa kujiunga nao kutokana na changamoto kadhaa zilizokuwepo wakati huo. Sasa nilipokuja tena hapa ikawa rahisi kumalizana nao kwani hata yale yaliyotukwamisha mwanzo hayapo,” amesema.


Ondoka na Mkwanja Kwenye Tsh. 160,000,000

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu.

Soma Zaidi

30 Komentara

    Ntibazonkiza amekuja kufanya maajabu ndani ya yanga

    Jibu

    Naamini ataleta mabadiliko yanga

    Jibu

    Vizuri atareta mafanyikio kwenye kikosi hicho

    Jibu

    tunasubiri kuona mabadiliko ya hali ya juu yanga

    Jibu

    Acha tuone kama wataweza

    Jibu

    Wataweza kweli

    Jibu

    Tunasubiri tuone mabadiliko yao

    Jibu

    Tunasubili tuone utendaji wake wa kazi akiwa yanga

    Jibu

    Kila lakheri said katika majukumu yako mapya

    Jibu

    Hebu ngoja tuone

    Jibu

    Ngoja kwanza tuone

    Jibu

    Tusubir matokeo

    Jibu

    Imeleta bonge la kocha yanga

    Jibu

    yanga ndio sehemu maalumu ya kuinua kipaji ukishanawili tu majirani lazima watakutolea macho juudi zako na nizamu yako ndio mafanikio yako piga kazi kijana hupo sehemu sahii

    Jibu

    Kazi kwenu yanga

    Jibu

    habar njema

    Jibu

    Kama nawaona wananchiiii

    Jibu

    Si kwl wachez wamekuwah watu wakudanya umma tujiulizeh kitu Kama KAzE asinge sain yanga je ntabazioka asingejiunga na yanga kwl all in all ngoj tuone uwanjan impact yake usajil mpya yanga

    Jibu

    Aonyeshe uwezo wake uwanjan

    Jibu

    Fresh tu

    Jibu

    Yanga hawajawah kukosea kwenye usajil wao

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Tunasubili tuone maujuzi yake

    Jibu

    Mungu waongoze mlete mabadiliko sasa

    Jibu

    Good

    Jibu

    Ata wamsajili nani bakola zipo pale pale

    Jibu

    Ngoja tujionee wenyewe

    Jibu

    Jembe limekuja kuleta mabadiliko Yanga

    Jibu

    Tunasubiri kuona kama yaliyomo yamo au

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.