Licha ya kwamba kocha – Mikel Arteta amemtema kwenye kikosi chake, bado Mesut Ozil anamapenzi na klabu ya Arsenal.
Ozil haijaitumikia Arsenal tangu Machi 7, 2020 na hayupo kwenye kikosi cha Arsenal kinachoshiriki michuano yoyote msimu huu.
Licha ya kwamba kiungo huyo angeweza kuondoka klabuni hapo, bado anasimamia msimamo wake wa kutumikia mkataba wake mpaka mwisho. Kutocheza mchezo wowote hakumfanyi Mesut kupunguza mapenzi yake kwa klabu hiyo.

Baada ya Arsenal kutolewa kwenye robo fainali ya Carabao Cup mchezo ambao umekamilisha vipigo 6 katika michezo 11, bado Mesut anaamini atapata nafasi kwenye kikosi hicho kinachotaabika kwa matokeo mabaya msimu huu.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Mesut ameandika “Ni wakati mgumu kwa kila mtu kwenye klabu – sio mimi tu. Ni kweli ninatamani ningeweza kuisaidia timu hasa wakati huu, lakini kutokana na kwamba sipewi nafasi, ninaimani tutapata matokeo mazuri siku chache zijazo.”
VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???



warda
Jamani anatia huruma
Shakila mrope
Kwanini lakini pamabana
Frank P
Biashara na utu vimeingilia mpira wake
Adelta
Mmmh! Vitu viwili tofauti
Rahmal
Duuh jamani kwa nn imekua ivo
Ernest Kimeru
Kuna muda unaweza ukawa unatafakari baadhi ya maamuzi kutoka kwenye uongozi wa vilabu mbalimbali na ukabaki na maswali mengi kichwani bila majibu, Ngoja tuone mwisho wake.
farida ahmad
Ozil Yuko sahihi
Saupha mohamed
Ozil yupo vizuri
Lydia Emmanuel Magoti
Ozil yupo sahii
Hopemwaikuka
Waache wakome wenyewe
Tatu
Ozil yupo sahihi
Sarah
Yupo vzr Ozil