Kieran Trippier Aadhibiwa Kukosa Mechi 14!

Mlinzi wa Atletico Madrid na Uingereza, Kieran Trippier amefungiwa kwa wiki 10 kujishughulisha na soka na anatakiwa kulipa faini ya £70,000 kwa kukiuka sheria za Shirikisho la Soka (FA) juu ya masuala ya Ubashiri.

Tamko la FA limethibitisha juu ya uamuzi huo wa kumsimamisha kwa wiki 10.

Nyota huyu mwenye miaka 30 hatatakiwa kushiriki kwenye shughuli zozote za kimichezo mara tuu baada ya hukumu hiyo kutoka, na athabu yake itadumu hadi Februari 28, 2021.

 atletico madrid kieran trippier
Kieran Trippier

Kieran Trippier alikuwa anatuhumiwa kwa makosa 7 yanayohusiana na kukiuka vipengele vya masharti ya sheria za FA (FA Rule E8 [1][b]) mwezi Julai 2019. Katika makosa hayo aliweza kukana makosa yote lakini makosa manne yalipatikana kuwa na ushahidi na kupelekea maamuzi ya adhabu hiyo.

Kutokana na adhabu hiyo, staa huyu atajikuta anakosa takribani mechi 14 za La Liga, na mechi moja ya mzunguko wa Ligi ya Mabingwa hatua ya mtoano wa timu 16 dhidi ya Chelsea.

Kwa maana hii, Trippier anatarajia kurejea tena dimbani wakati Atletico wakiwakaribisha Real Madrid kwenye El Derbi Machi 7.


 

VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???

SOMA ZAIDI

11 Komentara

    Duu sio poa

    Jibu

    Ni vizuri kwa wengine ili wajifunze

    Jibu

    pole yake jamani

    Jibu

    Mhh anatia huruma

    Jibu

    Aise majanga kweli pole yake

    Jibu

    Kieran Trippier mtukutu sana

    Jibu

    Jamaa mtukutuka sana

    Jibu

    Pengo kwa jose

    Jibu

    So sad

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

    Mh pole yake

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.