Tetesi zinasema Dortmund ina mpango wa kuwa na Haaland baada ya msimu huu, kulingana na mkuu wa kikosi cha kwanza cha soka, Sebastian Kehl. Vilabu 6 vinamuwinda ikiwemo Chelsea, City, United na Liverpool.
Arsenal inataka kumnunua mlinzi wa Brighton na England Tariq Lamptey, 20, na beki wa Norwich Muingereza Max Aarons, 21, kuchukua nafasi ya Hector Bellerin, 25, ambaye amehusishwa na tetesi za kujiunga na Paris St-Germain.
Chelsea itatia kibindoni asilimia isiyojulikana ya ada itakayopokewa na Brighton wakimuuza Lamptey baada klabu hizo mbili kukubaliana katika mpango ambao ulimwezesha mlinzi huyo kuondoka Stamford Bridge na kutua Seagulls Januari 2020.

Tetesi zinasema mgombea uraisi wa Barcelona Joan Laporta anataka mshambuliaji wa Manchester City na Argentina Sergio Aguero, 32, kujiunga na klabu hiyo msimu huu.
Mkufunzi wa Gunners Mikel Arteta amesema yupo makini kuiongoza Arsenal licha ya madai yanayomhusisha Barcelona lakini mazungumzo ya mkataba mpya utakaomwezesha kusalia Emirates hayajaanza.
Arteta anasema mazungumzo kuhusu kandarasi ya mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette,29, ambaye mkataba wake wa sasa na Arsenal unaendelea hadi 2023, yataanza hivi karibuni.
Tetesi zinasema Ashley Young, 35, anamatumaini ya kunyakua taji la Serie A na Inter Milan kabla ya kurejea klabu yake ya kwanza ya Watford kwa mkataba wa bila malipo msimu huu.

Tetesi zinasema meneja Jurgen Klopp amekiri kuwa Liverpool itakuwa na wakati mgumu kuwavutia wachezaji endapo haitafuzu kujiunga na Ligi ya Mabingwa.
Mkurugenzi wa AC Milan Frederic Massara amefichua kuwa klabu hiyo bado haijaamua ikiwa itaanza mazungumzo ya kumnunua Fikayo Tomori,23, lakini AC Milan inasisitiza bei ya £26m iliyotolewa na Chelsea iko juu sana.
Tetesi zinasema mkufunzi wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer ameonya juu ya kiwango cha pesa ambacho kitatumiwa na klabu hiyo msimu huu wa joto.
Ni Muda wa Kuvuna Mkwanja na Jungle Jim and the Lost Sphinx
Hauihitaji kufikira mara mbili ni mchezo gani utakupatia mkwanja ndani ya kasino za Meridianbet. Jiunge sasa ufurahie Jungle Jim and the Lost Sphinx.



Caroline
Asante kwa taarifa
Venerose
Asanteni kwa makala
Rahma
Ziko poa tetes
Adelta
Zimekaa vizuri
warda
Tetesi ziko poa sana
Mwanahamisi
Asante kwa makala
Hopemwaikuka
Zmeeleweka
Lydia Emmanuel Magoti
Tetesi zime kaa poa
Sarah
Zimesomeka