Wakati kukiendelea kuwa na hali ya sinto fahamu kuhusu uwezekano wa Cristiano Ronaldo kubeba kombe la Uefa akiwa na Juventus, Zinedine Zidane ameibuka na kuongeza chumvi.
Cristiano Ronaldo aliondoka Real Madrid 2018 baada ya kubeba mataji 3 ya msimu ule na alijiunga na Juventus. Lengo kuu la Juve kumsajili CR7 lilikuwa kubeba kombe la Uefa lakini mambo yamekuwa tofauti sana, Juve wameishia robo fainali mara 2 na kutolewa hatua ya 16 bora msimu huu.
Baada ya kuondolewa na FC Porto msimu huu, kulianza kuibuka maneno huenda CR7 akarejea Real Madrid huku wengine wakienda mbali na kusema usajili wa Ronaldo kwenda Juventus haukuwa sahihi.

Kocha Zinedine Zidane ametia chumvi kwenye hiki kinachoendelea ambapo Zizzou amenukuliwa akisema, ” Ndio, inawezekana ikawa ni kweli. Tunamjua Cristiano ni mtu wa aina gani na kila kitu alichokifanya hapa [Bernabeu]. Kwa sasa ni mchezaji wa Juve na tunapaswa kuheshimu hilo.
“Kwa sasa, tusubiri tuone nini kitatokea hapo mbeleni. Nilikuwa mwenye bahati kumfundisha na anajituma sana. Kwa sasa, anaisaidia Juventus“ aliiambia Sky Italia.
Maana Kamili ya Ushindi Katika Kasino za Meridianbeti ni Pamoja na Mchezo wa Tropical Wild.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Tropical Wild na uwe moja ya washindi na Mabingwa.



Caroline
Zidane yupo juu
Sarah
Zidane yupo vizuri
Venerose
Zidane namkubali
Hopemwaikuka
Maelewano tu
Neema juma
Zidane sio mtu wa mchezo mchezo
Lydia Emmanuel Magoti
Maerewano tuuu
Adelta
Inawezekana wakiamua
Dorophina
Kikubwa mpunga tu hapo
warda
Ronaldo aende Man U tu