Masumbwi: Pambano la AJ vs Fury Linanukia.

Moja pambano linasubiriwa na mashabiki wengi wa mchezo wa masumbwi/ndondi ni mtanange kati ya Anthony Joshua [AJ] vs Tyson Fury. Hili litatokea siku sio nyingi.

Kumekuwa na taarifa zinazokinzana mara kwa mara kuhusu uwezekano wa AJ kupambana na Fury katika mchezo ambao utaamua nani ni bingwa wa dunia kati ya mabondia hawa wawili.

Siku ya Ijumaa, Fury alinukuliwa akisema ameacha kufanya mazoezi ya kujiandaa na pambano hilo kwa kile alichodai kuwa wapo mbali sana kwenye kukubaliana baadhi ya mambo.

AJ (kulia), Fury (kushoto) wakiwa na mataji yao ambayo yatawekwa mezani endapo wawili hawa watachuana kumtafuta bingwa wa dunia.

Safari hii, promota wa AJ, Eddie Hearn amesikika akiimbia Sky Sport kuwa ” pande zote mbili zimeshasaini, kwa wiki chache zijazo tutakuwa tukifanya utaratibu wa kuapata eneo na kuamua tarehe ya pambano hili kubwa la masumbwi”.

Sambamba na hilo, Hearn aliiambia ESPN kuwa wanalenga kutangaza eneo la mpambano huo mwezi ujao na kwamba tayari wameshafanya mazungumzo na maeneo 8 katika nchi mbalimbali zilizopo Mashariki ya Kati, Asia, Ulaya Mashariki na Amerika.

Pambano la AJ vs Fury litakwenda kuweka mtaji yote manne (WBA, WBO, IBF na WBC) mezani ambapo mshindi atayabeba yote na kuwa bingwa wa dunia.


Maana Kamili ya Ushindi Katika Kasino za Meridianbeti ni Pamoja na Mchezo wa Tropical Wild.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Tropical Wild na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

CHEZA HAPA

8 Komentara

    Pambano la ukweli

    Jibu

    Pambano kali

    Jibu

    Big pambano

    Jibu

    Can’t wait for this

    Jibu

    Pambano litakuwa bomba

    Jibu

    Pambano kali

    Jibu

    Mpambano sio wa kukosa kabisa

    Jibu

    Litakuwa bonge la pambano

    Jibu

Acha ujumbe