Kunako klabu ya FC Barcelona, nyota wa timu hiyo, Lionel Messi ameendelea kuwa nguzo imara kwa vijana wa Catalunya msimu huu.
Barca walikuwa uwanjani jana usiku kupambana na Huesca katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Camp Nou.
Mpaka mwisho wa mchezo huo, ubao ulisomeka Barca 4 – Huesca 1 ambapo Lionel Messi alipachika magoli 2 na Antoine Griezmann akisaidiana na Oscar Mingueza walipachika goli 1 kila mmoja.

Ukiacha magoli mawili ya Messi, mchezaji huyo ameifikia rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Xavi Hernandez kwa kuitumikia Barcelona kwa jumla ya michezo 767. Hii inamaanisha kwamba, endapo Messi atacheza mchezo dhidi ya Real Sociedad jumapili hii, mchezaji huyo anakwenda kuweka historia ya kuwa mchezaji aliyeitumikia Barca kwa michezo mingi zaidi.
Baada ya ushindi wa jana usiku, Barca imepanda mpaka nafasi ya 2 ikiwa imezidiwa alama 4 na vinara wa La Liga – Atletico Madrid.
Maana Kamili ya Ushindi Katika Kasino za Meridianbeti ni Pamoja na Mchezo wa Tropical Wild.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Tropical Wild na uwe moja ya washindi na Mabingwa.



Caroline
Xavi yupo juu
Venerose
Hongera sana Messi
Hopemwaikuka
Messi kiboko
Neema juma
Safii sana Messi
Sarah
Messi kiboko
Lydia Emmanuel Magoti
Messi yupo vizuri
Dorophina
Pongezi kwake messi
warda
Kumbe Xavi anajua kuwapita kina Messi?