Mamic Jela Miaka Minne

Meneja na kocha wa klabu ya Dinamo Zagreb ya Croatia, Zoran Mamic amejiuzulu nafasi yake baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka minne na miezi nane, siku mbili tu kabla ya mechi ya marudiano kati yake dhidi ya Tottenham ya Mourinho kwenye Ligi ya Europa Alhamisi.

Mahakama kuu ya nchini humo imethibitisha pia kifungo cha miaka mitatu gerezani kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa zamani wa klabu hiyo, Dinamo Damir Vrbanovic.

Mamic na wenzie walikuwa wameshtakiwa kwa upigaji kupitia ukwepaji wa kodi wenye thamani ya pauni milioni 1.4 (Sh 4.5 Bilioni) na kujikusanyia jumla ya euro milioni 13 (Sh 36 Bilioni) kutoka kwenye uhamisho wa wachezaji.

Mamic amefunguka mara tu baada ya hukumu hiyo kuthibitishwa na mahakama, akisema:

“Ingawa najua sina hatia, lakini ninajiuzulu kama nilivyosema kabla ningefanya ikiwa hukumu hiyo itathibitishwa. Ninaitakia kila la heri klabu,” alisema Mamic.

Mabingwa hao wa Croatia wako nyumbani dhidi ya Tottenham Alhamisi hii katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Uropa raundi ya 16 baada ya timu hiyo ya Uingereza kushinda mchezo wa kwanza 2-0.


Maana Kamili ya Ushindi Katika Kasino za Meridianbeti ni Pamoja na Mchezo wa Tropical Wild.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Tropical Wild na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

CHEZA HAPA

9 Komentara

    Pole sana Mamic

    Jibu

    Sorry for him

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

    Duuh pole yake

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

    Pole Sana

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

    Duhhh atari sana

    Jibu

    Pole yake mamic

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.