PSG Kuivamia EPL Kwa Nyota Wawili.

Wakati mashindano ya Euro 2020 yakiwa yanaendelea barani ulaya, usajili wa dirisha kubwa nao unashika kasi. PSG kuivamia EPL kwa nyota wawili.

Imeripotiwa kuwa, Paris Saint Germain ina mpango wa kuzisaka saini mbili. Nyota wa Spurs, Harry Kane sambamba na kiungo wa Man United, Paul Pogba.

Mwishoni mwa msimu wa 2020/21, Kane aliweka wazi adhma yake ya kutaka kuondoka Spurs kwa kile alichodai ni anataka kucheza kwenye timu inayoweza kumpatia mataji. Licha ya mmiliki wa Spurs kuweka ugumu kwenye usajili wa Kane, inasemekana mshambuliaji huyu anaendelea kukasirishwa na mwenendo wa klabu hiyo ambayo mpaka sasa inasuasua kumpata kocha mpya.

Pauni milioni 150 ndio gharama iliyotajwa na Levy kwa anayetaka kumsajili, uwezekano wa Man City na Chelsea kumsajili Kane upo lakini ni suala gumu kwa Spurs kuruhusu Kane ajiunge na timu pinzani ndani ya EPL. Kwa PSG inawezekana kutokana na uwepo wa swahiba wake, Mauricio Pachettino lakini pia klabu hiyo haina uhakika sana na hatma ya Mbappe ambaye anahusishwa na Real Madrid.

Kwa Pogba ni dhahiri usajili wa Madrid haupo kwenye rada za mchezaji huyu baada ya Zinedine Zidane kuondoka klabuni hapo. Juventus napo hapaelewek, suala la uchumi ni kipengele kikubwa. Akiwa amesalia na mwaka mmoja pekee kwenye mkataba wake, Pogba anaweza kuondoka United ndani ya dirisha hili la usajili au United watamkosa kama mchezaji huru kuanzia mwezi Januari, 2022.

Ni PSG pekee wenye uwezo wa kumsajili Pogba majira haya ya joto endapo United hawatomuongezea mkataba na ipo wazi, kiungo huyo hanashida linapokuja suala la kuondoka United na miamba ya Paris imekuwa ikihusishwa nae kwa muda mrefu sasa, huenda huu ukawa ni muda wa kiungo huyu kurejea nyumbani.


SHINDA TSH 150,000,000/=

Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑

Atletico, Atletico Waunga Tela kwa Calhanoglu, MeridianbetINGIA MCHEZONI

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.