Rais wa klabu ya Barcelona Joan Laporta ameweka wazi kuwa haikuwa kazi rahisi kukamilisha uhamisho wa kocha wao mpya Xavi Hernandez kutoka kwenye klabu ya Al Sadd hasa kwenye kipindi hichi cha ukata wanachopitia.
Joan Laporta hakusafiri kwenda jijini Doha kufanya makubaliano na klabu ya Al Sadd kwenye uhamisho wa Xavi badala yake aliwatuma Mateu Alemany na Rafa Yuste kufanikisha uhamisho huo.

Uhamisho huo umechekua muda kukamilikia kutokana na ukata ambao klabu ya Barcelona inapitia, hadi kufikia hatua ya kumshawishi Xavi mwenye atoe kiasi fulani cha fedha ili kufanikisha uhamisho huo, Barcelona haikuweza kufanikiwa kuvunja mkataba ambao ulikuwa na thamani ya €5million peke yake.
Rais wa Barcelona Joan Laporta hakuweza kutoa maelezo kwenye utambulisho wa xavi, “kufanikisha kuondoka al sadd, klabu na xavi walishirikiana kuwa kitu kimoja na tumefanikiwa, haya ni maelezo kwa kifupi.” Alisema Laporta
Xavi sasa ni kocha rasmi wa klabu ya Barcelona na amshepewa mikoba ya kuiondoa nafasi ya tisa kurudi kwenye ushindani wake na kuhakikisha kuwa anaivusha kwenye klabu bingwa barani ulaya.
Unawezaje kuikosa hii! njia rahisi ya kutengeneza mkwanja katika kasino maridhawa za meridianbet. Muda wa kufurahia na kutengeneza mkwanja ipo mikononi mwako unasubiri nini?


