Wakati tukiwa tunahesabu masaa machache kukamilisha siku 365 za mwaka 2021, matukio ni mengi yametokea. Old Trafford kulikua na matukio yake mtambuka.
Manchester United imeendelea kumulikwa na vyombo vya habari kote ulimwenguni kutokana na ukubwa wake kama timu ya soka nchini Uingereza na Barani Ulaya. Mwaka 2021 umekuwa na matukio ya kila namna kwa miamba hii ya soka duniani. Haya ni baadhi;
Mbio za Ubingwa vs Man City – Msimu wa 2020/2021:
Wakati msimu wa 2020/21 unaanza, Man United wakiwa chini ya Ole Gunnar Solskjaer, hawakupewa nafasi kubwa kwenye mbio za ubingwa wa EPL. Baada ya nusu ya kwanza ya msimu kukatika, The Red Devils walirejea kwa kasi kwenye nusu ya pili.
United wakaanza kuonekana kama timu inayotafuta ubingwa kwa udi na uvumba. Nafasi ya 1 na 2 zikawa ni mbadilishano kati ya Manchester City na Manchester United. Msimu unaisha, City anabeba ubingwa huku United akishika nafasi ya 2 mbele ya Liverpool na Chelsea.

Kukosa Ubingwa wa Ligi ya Europa 2020/21:
Man United walishindwa kufua dafu kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa. Matokeo yake, wakateremka kwenye Ligi ya Europa. Safari yao kwenye Europa ilikua ni ushindi kwa kila mechi waliyocheza mpaka walipofikia fainali.
Solskjaer uso kwa uso na Unai Emery, dakika 120 zikakatika na mikwaju ya penati ikaamua bingwa. De Gea akakosa penati ya ushindi kwa United na ubingwa ukaenda kwa Villarreal.
Usajili dirisha kubwa – 2021/22:
The Red Devils wakajitosa na kuonesha misuli yao ya kifedha kwenye dirisha la usajili majira ya joto. Nyota watatu wakatua Old Trafford. Jadon Sancho, Rafael Varane na Cristiano Ronaldo wakaongezeka kwenye kikosi cha United ambacho tayari kilimtambulisha Tom Heaton kwenye idara ya magolikipa.
Manchester United ilimwaga pesa sokoni!! CR7 alihusishwa na kujiunga na Man City akitokea Juventus. Lakini, masaa mawili baada ya taarifa hizo kusambaa, ulimwengu ukashuhudia CR7 akirejea Old Trafford tangu alipoondoka mwaka 2009. “The Return of CR7”, ulimwengu wa soka ulisimama kwa muda kuwapisha mashabiki wa United kuitawala dunia.

“The comeback Kings” of 2021:
Pesa sokoni, mpira uwanjani. Msimu wa 2021/22 ukaanza, United wakiwa na nyota wake wote. Safari ya pili ya CR7 ilianzia Old Trafford alipotambulishwa kwenye mchezo dhidi ya Newcastle United. Kama kawaida yake, CR7 akazifumania nyavu mara 2 kwenye ushindi wa magoli 4 kwa United.
Matokeo ya United yalianza kusuasua, timu ikawa kazi yake ni kupindua meza. Ligi ya mabingwa ndio kielelezo kizuri, United walipindua meza kwenye michezo dhidi ya Villarreal na Atalanta huku CR7 akiokoa jahazi kwenye michezo yote miwili na kuivusha United hatua ya makundi.
Hali ikawa mbaya kwa United baada ya kupokea vipigo vikubwa kwenye EPL msimu wa 2021/22. Ikiwa ni mapema bado kwenye msimu, United alipigwa 4-1 na Leicester City, 5-0 dhidi ya Liverpool, 2-0 dhidi ya Man City na kwa aibu zaidi, United alipokea kipigo cha 4-1 dhidi ya Watford, timu ambayo imepanda daraja msimu huu na ikiwa kwenye orodha ya timu 3 zinazoshikilia mkia kwenye msimamo wa ligi.

Ole Gunnar Solskjaer Kusimamishwa Kazi Manchester United:
Licha ya kuwa miongoni mwa magwiji wa klabu, Ole Gunnar Solskjaer alijikuta akiikosa ajira yake baada ya bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo kumsimamisha kazi. Matokeo mabaya uwanjani, ilikuwa ni sababu ya Ole kuondolewa na timu kukabidhiwa kwa Michael Carrick kama muangalizi wa muda.
Carrick aliiongoza United katika michezo mitatu (Villarreal, Chelsea na Arsenal), alishinda michezo miwili na kutoa sare mchezo mmoja (dhidi ya Chelsea). Aliamua kuachana na timu hiyo baada ya mchezo dhidi ya Arsenal ambao ndio ulikua mchezo wake wa mwisho kama mfanyakazi wa Manchester United.

Ralf Rangnick Kupewa Timu Kama Kocha wa Mpito:
Wakati tayari United ikiwa imemuondoa Ole na Carrick kuamua kuondoka klabuni hapo, baadhi ya makocha kama vile Pochettino, Ten Hag na Brendan Rogers walihusishwa na kibarua kule Old Trafford. Mwisho wa siku, Ralf Rangnick akatolewa kwenye majukumu yake kule Lokomotiv Moscow na kukabidhiwa timu kwa mkataba wa miezi 6 kama kocha wa muda.
Maisha chini ya Rangnick yamekuwa ni mapya miongoni mwa mashabiki na wachezaji wa United. Mfumo wa 4-2-2-2 ni kitu kipya sana Old Trafford lakini ndio maisha chini ya Rangnick. Toka akabidhiwe timu mjerumani huyu, ameiongoza United kwenye michezo 4 akishinda michezo 2 na kutoka sare 2.
Man United wataufunga mwaka 2021 kwa mchezo dhidi ya Burnley leo usiku. Rangnick anamalizaje mwaka? Weka bashiri yako na Meridianbet!! Bofya hapa.
Unaanzaje siku yako katika msimu huu wa sikukuu, mchongo upo meridianbet kasino. Sloti pendwa ya Sahara Richies inaweza kukufanya ukawa milionea katika kufunga mwaka huu, Jiunge na ufurahie kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa.

CHEZA HAPA

