Nyota kutokea nchini Hispania Rafael Nadal ametua kwenye jiji la Melbourbe nchini Australia ili kushiriki michuano ya Australian Open baada ya kupona ugonjwa wa Uviko-19
nyota huyo wa kutokea Hispania mwenye umri wa miaka 35 aliwai kushinda michuano hiyo mwaka 2009, ameweka wazi leo kuwa amewasili jijini Melbourne baada ya kuchapisha picha yake kwnye mtandao wa Twitter akiwa kwenye uwanja ukiwa mtupu huku akiweka maneno, “usimwambie mtu ….. niko hapa.”
Mshindi mara 20 wa Grand Slam Rafael Nadal, alipatikana na maambukizi ya Uviko -19 baada ya kuwasili nchini kwao akitokea kwenye mashindano ya maonyesho jijini Abu Dhabi, wachezaji kadhaa walioshiriki michuano hiyo waligundulika kuwa na maambukizi ni Andrey Rublev, Belinda Bencic na Emma Raducanu.
Bado kuna wasiwasi mkubwa mchezaji namba moja wa dunia Novak Djokovic kama atakuwepo, sababu alijitoa kwenye timu ya serbia itakayoshiriki ATP Cup, huku pia akikataa kuweka wazi ikiwa kama amechanja au la.
Unaanzaje siku yako katika msimu huu wa sikukuu, mchongo upo meridianbet kasino. Sloti pendwa ya Sahara Richies inaweza kukufanya ukawa milionea katika kufunga mwaka huu, Jiunge na ufurahie kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa.

CHEZA HAPA


