Rudiger Kuwakacha PSG, Madrid Kunavutia.

Wakati Thomas Tuchel na bodi ya wakurugenzi wa Chelsea wakiwa na imani ya kubamkiza Antonio Rudiger, huenda wakaambulia patupu. Ni suala la muda tu.

Rudiger anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu na hali ilivyo kwa sasa, beki huyu kisiki hajakubaliana na mkataba mpya aliopatiwa na Chelsea. Inasemekana, suala la mshahara ndio changamoto.

Chelsea wameweka mkataba wenye mshahara wa £140,000 kwa wiki, hii ni pungufu ya mshahara anaoutaka Antonio (£200,000). Akiwa na umri wa miaka 28, beki huyu anaamini hii ndio fursa yake iliyosalia ya kupata mshahara mkubwa kwenye maisha yake ya soka.

Wakati The Blues wakisuasua kuongeza mshahara, PSG wameshaweka mezani ofa ya £6M kwa mwaka endapo Antonio atachagua kujiunga na timu hiyo kama mchezaji huru. Real Madrid nao hawapo nyuma katika hili, japokuwa inasemekana wameweka pesa pungufu kidogo ya ile ya PSG, lakini, Madrid ni Madrid.

Kwa hali ilivyo, ripoti zinasema. Rudiger hana mpango na kwenda Ufaransa. Moyo na akili yake ipo kwenye majiji mawili tu – London na Madrid. Hii inamaana kuwa, Chelsea wajiongeze au ajiunge na Real Madrid mwishoni mwa msimu huu.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.