Bondia wa Mexico Canelo Alvarez,31, amepoteza kwa pointi pambano lake dhidi ya Mrusi Dmitry Bivol,31, ambaye ametetea ubingwa wake wa taji la WBA light Heavyweight.

Canelo Apoteza kwa Pointi Dhidi ya Bivol

Pambano hilo la raundi 12 lilifanyika usiku wa kuamkia leo T-Mobile Arena-Nevada nchini Marekani. Majaji wote watatu walimpa Bivol Pointi 115-113. .Hii ni mara ya kwanza Canelo anapoteza pambano tangu mwaka 2013, alipopoteza dhidi ya Floyd Mayweather.

Lakini aliongea baada ya pambano hilo kuisha Canelo alisema: “Unapaswa kukubali, ndiyo ndondi,” Alvarez. “Ni bingwa mkubwa muda mwingine kwenye ndondi unashinda au kupoteza, sijitetei nimepoteza na yeye ameshinda.

Dmitry Bivol sasa ameshinda mapambano yake yote 20 aliyopigana, 11 akishinda kwa KO.

Canelo mpaka sasa amecheza mapambano 61, akishinda 57 (39 kwa KO), sare mawili na kapoteza mara mbili.

Aliulizwa kama kuna uwezekano wa kama anania ya pambano la marudiano Canelo alisema: “Ndiyo nina nia, haiwezi kuishia kama hivi.

Huu siyo mwisho najijua mimi ni mshindani sana na nina muda mwingi wa kuendelea na mchezo hivyo nitarudi nikiwa na nguvu.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa