Tambo za Wilder Akimsubiri Breazeale

Bingwa wa dunia wa ndondi za uzani wa juu Deontay Wilder anatarajiwa kutetea ubingwa wake dhidi ya Dominic Breazeale kule Newyork mwezi Mei.

Pambano la Barclays Center liliamuliwa na WBC baada ya Briton Tyson Furry kuamua kuchukua pambeno jingine baada ya kufanya pambano la marudiano na Wilder.

Bingwa ambaye Wilder anaendea kupambana naye, Breazeale amepoteza pambano moja tu katika mapambano yake 21, alipoteza pambano lake na bingwa wa IBF, WBO na WBA Anthony Joshua.

Deontay anamtambia mpinzani wake kuwa atamuonesha kazi siku ya pambano. “ninashikilia funguo, nitamtandika huyu mpuuzi”

Breazeale naye anasema kuwa anataka kuhakikisha anampokonya taji, anajitambua yeye ni mpiganaji mkubwa lakini kila siku kuna kitu cha kujifunza kwa hiyo anatumia kila nafasi anayoipata kujifunza.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.