Mpiganaji wa ndondi mchanganyiko McGregor aliwekwa kizuizini na na polisi wa America baada ya kuripotiwa alipokonya na kuivunja kwa makusudi simu ya shabiki nje ya klabu ya usiku ya Florida.
Mpiganaji huyu mwenye umri wa miaka 30 alikuwa na shtaka la unyanganyi wa kutumia nguvu baada ya kuchukua suimu hiyo ya shabiki na kuipasua. Polisi wa Miami walidai kuwa waliitwa eneo la tukio mida ya saa kumi na moja asubuhi nje ya klabu ya usiku ya LIV.
Baada ya kuanza uchunguzi McGregor alikamatwa na kuwekwa kizuizini Miami-Dade. Dhamana yake iliwekwa kwa $12 500
Kwa mujibu wa ripoti, shabiki ambaye simu yake ilipokonywa na alijaribu kumpiga picha McGregor kwa simu yake ambayo inatyajwa kuwa na thamani ya $1 000. Baada ya maywether, kuichukua simu hiyo na kuidua juu yake, aliondoka nayo bila kuirudisha.
Staa huyu ni anafahamika zaidi kwa pambano lake alilopoteza kwa Floyd Mayweather, camera zilizotegwa maeneo ya kumbi hiyo zilimnasa McGregor akifanya tukio hilo.
Shabiki anasimulia kuwa McGregor aliitandika ngumi simu yake, aliihisi ngumi ile kwenye mwili wake. Alipotaka kichukua simu yake ambayo ilikuwa imedondoka Mcgregor akaichukua yeye na kuibamiza tena chini kabla hajaikanyaga kama mara 4 kisha akatokomea zake na simu.
Huyu jamaa, ni mwanandondi ambaye hupenda kufanya mazali ya rejareja, alishawahi kuvamia basi lililokuwa na wapinzani wake kadhaa na kuwatupia chuma, kosa lililomuacha na adhabu ya kifungo cha nje na adhabu ya kupata mafunzo ya kuzuia hasira.


Furahav
Hii sio poa.