Barcelona: Reverter Kuachia Nafasi ya Ukurugenzi wa Klabu

Barcelona wametangaza kuwa mkurgenzi mtendaji Ferran Reverter atajiuzulu wadhifa wake baada ya miezi saba pekee kwa sababu binafsi na za kifamilia.

Barcelona: Reverter Kuachia Nafasi ya Ukurugenzi wa Klabu

Reverter alichukua nafasi hiyo Julai mwaka jana na alipewa jukumu la kupunguza deni la klabu lililokuwa likiongezeka na kuandaa mradi wa kutengeneza upya Camp Nou.

Lakini Reverter mwenye umri wa miaka 49, ambaye alimrithi Oscar Grau miezi mitatu baada ya Joan Laporta kuchukua wadhifa wa rais wa klabu, anatarajiwa kutoa nafasi kwa Mkurugenzi Mtendaji mpya.

Barca walitangaza habari hizo kwenye tovuti yao rasmi Jumanne, huku wakithibitisha kuwa Reverter atasalia kwenye nafasi hiyo hadi atakapopatikana mbadala wake.

Reverter alisema katika taarifa yake: “Sasa ni takriban mwaka mmoja tangu niondoke Ujerumani kurejea Barcelona kwa sababu za kifamilia na muda mfupi baada ya kukubali ofa niliyopokea kutoka kwa rais Joan Laporta ya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa klabu.

“Binafsi nimeweka juhudi nyingi na kujitolea katika miezi hii, lakini sasa nataka kuangazia sababu iliyonifanya nirudi Barcelona, ​​ambayo ni kutumia muda mwingi katika miradi yangu binafsi na familia.”


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.