Hiki ndiyo kipindi ambacho Martin Braithwaite ana nafasi kubwa ya kucheza katika kikosi cha Kwanza cha Barcelona baada ya kuondoka kwa Lionel Messi na Antoine Griezmann wakati wa dirisha la usajili.

Lakini, kutokana na kupata jeraha wakati wa mechi dhidi ya Getafe mwezi Agosti 29, kabla ya mapumziko ya mechi za kimataifa sasa analazimika kukaa pembeni kuelekea michezo ya hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa Barcelona watakapo wakaribisha Bayern Munich.
Barcelona ilitangaza siku ya Jumatatu asubuhi kwamba Braithwaite atapaswa kufanyiwa upasuaji siku chache zijazo kutokana na shida ya mguu wake wa kushoto.
Inakadiriwa kwamba fowadi huyo wa miaka 30 atakuwa nje ya dimba kwa muda wa miezi miwili mpaka minne ingawa klabu imesema itaweka wazi mara baada ya operesheni kukamilika.
Kumpoteza Braithwaiteimekuja katika kipindi kigumu sana kwa Barcelona ambapo wana idadi kubwa ya majeruhi, ambao ni Ousmane Dembele, Ansu Fati, na Sergio Aguero.
Kwa hiyo Memphis Depay, Yusuf Demir na Luuk de Jong watapaswa kufanya kazi nzuri katika mchezo wao na Bayern Munich siku ya Jumanne.
Unaanzaje siku yako na kuimaliza bila kupitia katika kasino bomba za meridianbettz, mchezo mashuhuri wa Disco Funk unaweza kukufanya uwe mshindi leo hii.!


