Kocha wa Wolves Bruno Lage amechaguliwa kuwa Meneja Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu ya Uingereza Januari 2022.

Mtaalamu huyo wa Ureno aliwasili Molineux majira ya joto kama mrithi wa Nuno Espirito Santo na amefanya kazi nzuri huko West Midlands hadi sasa.
Baada ya kushinda mechi zao zote tatu za Ligi Kuu mwezi Januari, Lage ameshinda tuzo yake ya kwanza ya Kocha Bora wa Mwezi msimu huu.
Wolves walianza mwezi kwa ushindi maarufu wa 1-0 dhidi ya Manchester United lililofungwa na Joao Moutinho dakika za lala salama. Kisha wakamaliza Januari kwa ushindi nyumbani kwa Southampton na ugenini wakiwa Brentford.
Wakati huohuo mlinda mlango wa Manchester United David de Gea pia ameshinda mchezaji bora wa mwezi Januari, Mlinda mlango huyo wa Red Devils aliokoa michomo 22 mwezi uliopita tano zaidi ya mtu mwingine yeyote.
De Gea ametunukiwa taji la Mchezaji Bora wa Mwezi pamoja na kadi maalum ya FIFA 22 ya EA Sports.
Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.


