Chelsea wanasubiri ukamilisho wa kuuzwa kwa klabu hiyo ili waweze kusajili wachezaji na Jules Kounde anapewa kipaumbele cha kuletwa Darajani haraka iwezekanavyo.

Kufuatia kuodoka kwa Antonio Rudiger kwenda Real Madrid na Andreas Christensen kwenda Barcelona, The Blues wanataka kuimalisha safu ya ulinzi hasa beki ya kati.

Chelsea na Sevilla wote wanania ya kukamilisha dili hiyo ili waweze kupata mbadala wake iliaweze kuzoea kasi na aina ya mpira wa Sevilla .

Kounde mwenye umri wa miaka 23 tayari amefanya makubaliano binafsi na Chelsea juu ya uwezekano wa kutua darajani msimu huu baada ya dili hiyo kufa mwaka jana.

Klabu hiyo wa Liga wanahitaji kukusanya takriban pauni milioni 38 ($47m) kusawazisha vitabu kabla ya Juni 30. Hata hivyo, wanaomba kiasi cha pauni milioni 59 ($73m) kwa ajili ya beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa, ambaye anaweza kucheza kama beki wa kati au wa kulia- nyuma.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa