Klabu ya Chelsea inaomba amani kufuatia vita ya Urusi dhidi ya Ukraine ambapo imepelekea watu kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa vilevile kuwa na athari mbaya kiuchumi.

Mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich alichukua uamuzi wa kujiuzulu baada ya kuhusishwa kuwa na uhusiano na rais wa Urusi Vladimir Putin na bilionea huyo wa Urusi na Israel alitangaza Jumamosi kuwa alikuwa akikabidhi “usimamizi na utunzaji” wa Chelsea kwa wadhamini wa msingi wa klabu, lakini atasalia kama mmiliki.

Uvamizi wa Urusi kwa jirani yake umeingia siku yake ya nne Jumapili, huku mapigano makali yakiripotiwa mjini Kharkiv, mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine.

Maoni ya kwanza ya Chelsea kwa umma kuhusu mzozo huo yalikuja saa chache kabla ya kumenyana na Liverpool kwenye fainali ya Kombe la Carabao kwenye Uwanja wa Wembley.

Taarifa hiyo ilisema: “Hali ya Ukraine ni ya kutisha na ya kusikitisha.

“Mawazo ya Chelsea FC yako kwa kila mtu nchini Ukraine. Kila mtu kwenye klabu anaombea amani.”


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa