Kiungo wa kati wa Milan Brahim Diaz amepima na kuapatikana na virusi vya coronavirus kabla ya mechi ya Serie A dhidi ya Hellas Verona siku ya Jumamosi.

Diaz, 22, anajisikia vizuri wakati anajitenga nyumbani, kulingana na taarifa kutoka katika klabu.
Hakuna wachezaji wengine waliokutwa na maambukizi katika raundi ya hivi karibuni ya vipimo kabla ya mechi ya Verona huko San Siro.
AC Milan, hata hivyo, tayari hawawtakuwa na beki Theo Hernandez kutokana na COVID-19 pia.
“Ufuatiliaji wa karibu na vipimo utafuata kulingana na dalili zilizotolewa na mamlaka husika za afya, ambao waliarifiwa mara moja,” ilisema taarifa ya Milan.

Diaz amecheza mechi zote saba za ligi za Milan msimu huu, akianza sita, na ingetarajiwa tena kutajwa kwenye XI dhidi ya Verona na kocha mkuu Stefano Pioli.
Mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid amefunga mabao matatu kwenye Serie A.
Fanya wiki yako iwe ya kuvutia zaidi, tunaelekea Los Angeles kutengeneza mkwanja na kasino maridhawa ya LA Rouge kutoka katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Fursa ya kufurahi huku unajaza pochi yako.

CHEZA HAPA

