Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, hatasaini mkataba mpya Paris St-Germain haijalishi klabu hiyo ya Ligue 1 itamlipa kiwango gani cha fedha kwani nyota huyo ameamua kuelekea Real Madrid.
Tetesi zinasema, Liverpool, Manchester City na Manchester United wanamnyatia kiungo wa kati wa Monaco na Ufaransa Aurelien Tchouameni, 21, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa karibu £40m.

Tetesi zinasema, Manchester City wanapanga kujaza pengo litakaloachwa na mshambuliaji wa England Raheem Sterling, 26, na mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 33.
Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amekubali kuwa kiungo wa kati wa England Jesse Lingard, 28, huenda asishawishike kusaini mkataba mpya katika klabu hiyo mpaka apatiwe muda zaidi wa kucheza.
Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa Everton na England Dominic Calvert-Lewin, 24, ni chaguo la kwanza la Arsenal msimu ujao.

Tetesi zinasema, Mkufunzi wa Roma Jose Mourinho anataka kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona Riqui Puig, 22, ambaye hana namba pale Nou Camp.
Beki wa Ujerumani Antonio Rudiger ameghadhabishwa na ofa ya Chelsea ya hivi karibuni. Mkataba wa sasa wa nyota huyo wa miaka 28-unamalizika mwisho wa msimu huu.
Kocha wa zamani wa Shakhtar Donetsk na Roma Paulo Fonseca ameibuka tena na anapigiwa upato kujiunga na Newcastle, ambayo inatarajiwa kumtimua Steve Bruce ndani ya wiki chache zijazo.
Fanya wiki yako iwe ya kuvutia zaidi, tunaelekea Los Angeles kutengeneza mkwanja na kasino maridhawa ya LA Rouge kutoka katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Fursa ya kufurahi huku unajaza pochi yako.

CHEZA HAPA

