Dili ya Militao Kwenda Madrid Kuchunguzwa

Mwendesha mashtaka wa umma wa Ureno ameripotiwa kuanzisha uchunguzi juu ya euro milioni 9.72 katika sehemu ya makubaliano ya euro 50m kati ya Porto na Real Madrid kwa Eder Militao.
Dili ya Militao Kwenda Madrid Kuchunguzwa
Eder Militao

Porto ilinunua asilimia 90 ya haki za Militao kutoka Sao Paulo kwa euro 8.5m mwaka 2018 na, mwaka mmoja baadaye 2019, Real Madrid ilinunua asilimia 100 ya haki zake kwa euro 50m, na Porto ikipata faida ya euro 38.16m.

Kwa mujibu wa gazeti la Ureno la Publico, asilimia 20 ya faida ya Porto ilielekezwa kwa mawakala wawili ambao wanachunguzwa. Ambao ni Giuliano Bertolucci na Bruno Macedo, ambaye alikuwa mmoja wa Wareno wanne waliokamatwa katika operesheni ya polisi iliyomlazimisha rais wa Benfica Luis Filipe Vieira kujiuzulu.

Wakati huo huo, mwendesha mashtaka pia anachunguza uhamishaji wa Militao kutoka Sao Paulo kwenda Porto, na mmoja wa wahusika wa kati ni Pedro Pinho, mfanyabiashara aliye karibu sana na rais wa Porto Jorge Nuno Pinto da Costa – ambaye alishtakiwa kwa kushambulia mpiga picha wa runinga ya Ureno TVI miezi michache iliyopita.

Kama ilivyoripotiwa na Publico, Pinho pia alikuwa mshirika wa kibiashara na Alexandre Pinto da Costa, mtoto wa rais wa sasa wa Porto.


JIUNGE NA FAMILIA YA MABINGWA!

Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!

Italia, Italia Bingwa Euro 2020., Meridianbet

JIUNGE SASA!

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.