Pierre-Emerick Aubameyang amevuliwa jukumu la kuwa kiongozi/nahodha wa timu ya Arsenal na hatokuwa sehemu ya mchezo wa Arsenal dhidi ya West Ham katikati ya wiki hii.

Aubameyang hakujumuishwa kwenye kikosi kilichomenyana na Southampton wikendi iliyopita wakati Arsenal ilipopata ushindi mnono wa 3-0 sababu ya utovu wa nidhamu.
“Tunatarajia wachezaji wetu wote, haswa nahodha wetu, kufanya kazi kwa sheria na viwango ambavyo sote tumeweka na kukubaliana,” klabu hiyo ilisema.
Maamuzi hayo yalikuja muda mfupi baada ya mwandishi wa Skysport Paul Merson akimuongelea Aubameyang kwamba Arsenal wanahitaji nahodha mwingine kutokana na mwenendo wa tabia ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Gabon.
Merson alisema “Hii siyo mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kufanya jambo kama hilo. Kuwa nahodha wa Arsenal ni heshima kubwa.
Kocha mkuu wa Arsenal Mikel Arteta anatarajia kufanya mkutano na waandishi wa habari siku ya leo kuelekea mchezo dhidi WestHam United.
Fanya wiki yako iwe ya ushindi mkubwa ndani ya kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo wa BURST THE BANK🔥🤑 ni moja kati ya mchezo pendwa unaowapa wachezaji mamilioni kila siku. Kwa dau dogo unashinda zaidi.


