Beki na Nahodha wa Yanga, Lamine Moro alitimuliwa wakiwa kambini Ruangwa wakijiandaa na mchezo wa VPL dhidi ya Namungo FC uliomalizika 0-0 na kurejeshwa Dar kwa madai ya utovu wa nidhamu.
Baada ya hapo kocha mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi aliutaka uongozi kuingilia kati akidai nyota huyo alionyesha utovu wa nidhamu wakati timu ikiwa katika maandalizi ya mchezo huo.
Mkuu wa Idara ya Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, amesema kuwa tayari uongozi umekaa na beki huyo kumsikiliza pia madai yake.
“Tulikaa na Lamine wiki iliyopita tukamsikiliza, kwa kuwa jambo lake alilileta kwetu basi tumelitatua na kumpa majibu yeye na kocha kama mkuu wa ufundi,” alisema Bumbuli.
Bumbuli amesema, licha ya kumaliza tofauti hizo bado nyota huyo hakuwa kwenye mipango ya kocha wao katika mchezo uliochezwa juzi Uwanja wa CCM Kambarage, mjini Shinyanga.
Amesema kila kitu kitakaa sawa mara baada ya timu kurejea kutoka Shinyanga.
Licha ya Nabi kudai kamfukuza kambini kutokana na utovu wa nidhamu, nyota huyo raia wa Ghana alikana na kusema kuwa yeye sio mtovu wa nidhamu, kocha aliona kama anamdharau lakini sio kweli.
BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.
Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.
Iwe fundisho kwa wengine