Klabu ya Newcastle imeingia katika kinyang’anyiro cha kumsajili mchezaji wa Barcelona ambaye yupo kwa mkopo katika klabu ya Aston Villa Philippe Coutinho.

Coutinho amekuwa kwenye vitabu vya Barca kwa miaka minne iliyopita, baada ya kukamilisha uhamisho wa pesa nyingi kwenda Camp Nou kutoka Liverpool Januari 2018.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil amebakiza mwaka kuendelea kuvaa jezi ya The Blaugrana lakini yupo tayari kurejea katika Premier League.

Klabu anayoichezea kwa sasa Aston Villa wana kipengele cha kumnunua moja kwa moja kwa kitita cha €40m (£34m/$42m katika mkataba wao wakati wa dirisha la usajili la majira ya kiangazi.

Na kocha wa sasa wa Villa Steven Gerard ambaye alicheza na Coutinho miaka ya 2013-15 wakati wakiichezea Liverpool amesema anataka kiungo huyo kusalia Villa Park.

Lakini Newcastle wapo tayari kulipa kiasi kama ambacho Villa wanataka kulipa ili waweze kumnasa na tayari wamefanya mawasiliano na Barca juu ya uwezekano wa kumsajili Coutinho.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa