Nyota wa Manchester United Christiano Ronaldo amemtetea mtoto wake Ronaldo Jr katika mtandao wa Instagram baada ya kinda huyo kukosolewa kwa kuchanganya brand za mavazi.
Ronaldo Jr alikuwa kwenye picha na bibi yake (mama wa Ronaldo) Maria Dolores ambaye aliweka picha kwenye akaunti yake ya Instagram ikionyesha mtoto huyo akiwa amevalia mavazi yenye chapa ya Nike na Adidas.
Inajulikana wazi kwamba Ronaldo ana udhamini mkubwa na kampuni ya Nike hivyo komenti nyingi zilikuwa zikimkosoa mtoto huyo kwa kuchanganya chapa lakini mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid alijibu maoni ya kwa kumtetea mwanae.
Ronaldo alisema “ Anavaa chochote anachokitaka siyo mnachokitaka nyie,”
Mkataba wa Ronaldo na Nike ni wa maisha na wenye thamani ya paundi milioni 780 (dola bilioni 1) kwa ujumla.
Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.