Baada ya EPL kusimama kwa wiki moja sababu ya mechi za kimataifa sasa wiki ya nane inaendelea leo Jumamosi ambapo Brentford watawaalika Chelsea ambapo ni mechi ya Debi ya London.
Chelsea watakuwa na lengo la kuendelea kubaki kileleni mwa ligi hiyo baada ya kushinda kwa 3-1 dhidi ya Southampton wakati Brentford waliinyuka 2-1 West Ham.
Taarifa ya Timu
Brentford, Mads Sorensen na Josh Dasilva wataendelea kutopatikana wakati Shandon Baptiste ambaye alitolewa katika kipindi cha kwanza kwenye mechi dhidi ya West Ham baada ya kuumia bega hatahusika katika mchezo wa leo.
Mathias Jensen ataanza eneo la kiungo lakini Kristoffer Ajer na Vitaly Janelt wanaweza kurejea baada ya kusumbuliwa na tatizo la paja.
Chelsea, watamkosa mlinzi wao Thiago Silva ambaye alikuwa katika majukumu na timu ya taifa wakati Reece James na N’Golo Kante wamerejea mazoezini baada ya kupona shida ya kifundo cha mguu.
Lukaku alikuwa kwenye shaka kubwa ya kukosa mchezo huu baada ya kuondolewa kwenye kikosi cha Belgium lakini Thomas Tuchel alithibitisha straika huyo atacheza dhidi Brentford.
Kikosi cha Brentford kinachoweza kuanza: Raya; Ajer, Jansson, Pinnock; Canos, Norgaard, Onyeka, Janelt, Henry; Toney, Mbeumo
Kikosi cha Chelsea kinachoweza kuanza: Mendy; Azpilicueta, Chalobah, Christensen; James, Jorginho, Kante, Chilwell; Mount, Havertz; Lukaku
Fanya wiki yako iwe ya kuvutia zaidi, tunaelekea Los Angeles kutengeneza mkwanja na kasino maridhawa ya LA Rouge kutoka katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Fursa ya kufurahi huku unajaza pochi yako.

CHEZA HAPA

