Bingwa mara nne kwenye mashindano ya F1 Sebastian Vettel anaamini Michael Masi anapaswa kubakishwa kwenye nafasi yake ya ukurugenzi wa mashindano japokuwa alifanya maamuzi ya utata kwenye fainali ya mashindani hayo 2021.
Masi yupo kwenye shinikizo kubwa baada kushutumiwa kupindisha sheria ili kuruhusu max kuweza kumshinda hamilton kwenye ubingwa wa jumla wa mashindano ya F1 yaliofanyika Abu Dhabi.
Mkuregenzi wa chama cha madereva wa Grand Prix Vettel ametoa shutuma hizo alipokuwa kwenye maonesho ya gari jipya la tumu ya Aston Martin alinukuliwa akisema, “Michael imekuwa mbaya kwake, kuna mvutano wa mambo mawili, moja ni mchezo na nyingine ni maonesho.”
“Michael amekuwa akijizatiti kufanya kazi nzuri, sifahamu ni nini kimehifadhiwa kwa baadae lakini natumai atasimama tena kwasababu ya vyote alivyofanya, kuna mambo mengi ya utata yamekuwepo kwenye mbio za mwisho, lakini haipaswi kuwa hivyo, kwa sababu ukiangalia kwa picha kubwa kwa aliyoyafanya, amefanya vizuri.”
Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.