Licha ya kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa mbio za langalanga mwenye mafanikio makubwa. Lewis Hamilton ni mwanaharakati wa haki za binadamu na mambo ya mazingira.

Kuelekea mbio za Bahrain Grand Prix, tayari wabunge 30 wa Uingereza wamezungumzia vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu ambavyo vinahusishwa na mbio hizo.

Hamilton amesema ameshapokea barua kadhaa kutoka kwenye makundi yanayopigania haki za binadamu ikiwa ni muda mfupi tangu alipofika Bahrain, Lewis amesema “nitatenga muda ili niweze kuzisoma zote kwa kina”.

Hamilton, Hamilton “F1 Waongeze Nguvu Kwenye Haki za Binadamu”, Meridianbet
Lewis Hamilton alitwaa taji la 7 kwenye F1 mapema mwezi huu.

“Ni muhimu sana kwa kila mchezo kutumia nafasi iliyonayo kubadilisha maisha ya watu. Haki za binadamu ni tatizo kila sehemu tunayokwenda.

“Sisi ni wanamichezo wachache ambao tunakwenda nchi nyingi na nina amini kama wanamichezo tunatakiwa kufanya kazi ya ziada.

“Tumeshapiga hatua katika uelekeo sahihi lakini bado tunapaswa kuongeza juhudi zaidi. Wameweka hatua za kufuata kwenye kila sehemu tunayokwenda lakini tunapaswa kuhakikisha hatua hizo zinafuatwa katika njia iliyo sahihi kiutekelezaji.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

17 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa